Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Kwanini huwa mnapenda kutumia KIFO na KUKATIKA PUMZI kama defend ya uwepo wa Mungu?

Hatuna point nyengine ZAIDI YA KIFO?

#YNWA
Hatujui tulipotoka, tunajua tulipo, hatujui tunapokwenda. MUNGU yupo akilini mwetu kurahisisha matumaini ya yale yasiyojulikana. Kifo hakijulikani, siri zake hazijulikani. Au ww unazifahamu?
 
Tulia anza kufikiria kulima nyanya na vitunguu ukauze, kama huna kazi. Supernatural power ipo. Mungu aliumbwa na nani, haitaondoa fact kwamba Mwenyezi Mungu yupo. Na ipo siku kama wasafiri, tutaondoka hapa duniani
 
Mtu akisoma hoja zako kwa makini atagundua kuwa, umeenda Chuo Kikuu wakati hujamaliza hata Chekechea.
Ungeanza kwanza kujibu maswali mengine mengi kabla ya kumfikia Mungu
Mfano wa baadhi ya maswali;
1. Nani aliumba watu/viumbe wengine kama wanyama na miti
2. Nani aliumba Milima, Moto, hewa nk
3. Nani aliumba maji (bahari)
4. Nani aliumba dunia, Jua na sayari nyingi unazozifaham kama unaelimu ya Jiografia au Fizikia

Ukishamaliza kufikiria vyote hivyo kwa makini na sio kijuu juu;
Utagundua kuwa Binadamu ni kitu kidogo sana kwenye uumbaji; kwani kulikuwa na complex structure kabla hata ya kuwepo kwa Binadamu la sivyo, Binadamu hangeweza kuishi huku duniani (mfano bila Jua, maji, hewa, chakula nk ). Siamini kama kuna mtu aliyesoma anaweza kuwa Mbumbumbu kiasi cha kufikiri kuwa, Binadamu aliyeko ndani ya dunia aliyoikuta ikiwa na kila kitu, eti naye ni muumbaji?
Mwanadamu huyu, ambaye hata hawezi kujua siku ya kufa kama sio kuzuia basi kifo? shame!!!
Sasa kwa kifupi
Hiyo Nguvu iliyofanya Dunia na vilivyomo ndani ya dunia, na uwepo wa Sayari Nyingine likiwepo Jua, ndiyo huitwa MUNGU
Mungu ni mmoja tu, na sio Kiumbe kwani hajaumbwa, hana mwanzo wala mwisho (kwa kuwa alikuwepo jana leo na hata milele), Hajazaa wala hajazaliwa (kwa hiyo hafi)
 
Ni kawaida yenu.

Huwa mnatumia vitisho kumaliza hoja zenu.

Kama serikali, ikiona mmezidi "Wanawatumia vitisho tu ili muogope"

Na hasa misikitini kumejaaa vitishoooo tu vya kifooo yaani ni full vitishoooo.

Haya nishaogopa NANYAMAZA.

#YNWA
Uzuri ukiogopa au usiogope ukitishika au usitishike uhalisia ni kwamba sote tunakufa so tujiandae.
 
Mungu ni jinga sana...linashindwa kujiweka wazi linajificha uko machakani linaacha mazombi yake ndio yanalitetea halafu cha ajabu na menyewe hata hayajiongezi hehehehe endeleen kumtetea huyo kima wenu.
 
Asilimia Tisini na tisa ( 99% ) ya wanadamu duniani wana mwamini Mungu kwa HOFU za kidini..si kwamba wana amini Mungu yupo kwa moyo wao wote bali wanahofia endapo wasipo amini kulingana na mafundisho yao ya kidini eti wakifa watachomwa moto milele.

Binadamu wanamwamini Mungu kwa hofu za kidini tu...ila nina uhakika asilimia mia moja wanadamu wote huwa wana jiuliza huyu Mungu mwenye huruma na upendo wa kweli kama mafundisho yao yanavyo wafunza Yupo kweli????
 
Mungu ni jinga sana...linashindwa kujiweka wazi linajificha uko machakani linaacha mazombi yake ndio yanalitetea halafu cha ajabu na menyewe hata hayajiongezi hehehehe endeleen kumtetea huyo kima wenu.
Hii komenti yako wafia dini na walokole waki iona watakushushia mvua ya matusi [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Binadamu ndio mwenye kuitafuta imani, ni wewe utakaye itafuta imani na Wewe ndiye wa kumtafuta Mungu, Mungu amesha kuumba na kukupa akili na maarifa .. , anakujua wewe ni mtoto wake, sasa utachagua imani ipi yakufaa zaidi.....!!!!
Dini zipo nyingi na hapo pia katika hizo dini kulikuwa na maslahi binafsi,

LAKINI IMANI YA MUNGU NI MOJA TU , kama WAAMINI Mungu muombe akuoneshe imani sahihi ni ipi???

Assignment nayo kuachia ni kumtafuta Mungu wako kwa bidii yote [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hii komenti yako wafia dini na walokole waki iona watakushushia mvua ya matusi [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Yan watu wamekuwa misukule kwenye hii miimani ya ajabuajabu...
acha waendelee kuburuzwa na hilo limungu lao.
 
Hii komenti yako wafia dini na walokole waki iona watakushushia mvua ya matusi [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Hakuna haja ya kumtukana huyo... Hata amtukane Muumba wake haipunguzi wala kuongeza chochote kwenye utukufu wa Muumba Mbingu na ardhi na vyote vilivyomo... Vinavyoonekana na visivyoonekana. AHSANTE
 
Kiranga wachungaji walimkimbia ila nachojua ni kwamba man created god is their own image,issue ya mungu ni uongo wa zama na zama.
Ishu ya Mungu ni Uongo... Je ulijiumba mwenyewe!? Mfano maji ni kitu muhimu sana kwa ajili ya uhai wetu.. Je haya maji uliyaleta WEWE(AU KIBURI TU NDUGU YANGU??)
 
Nikuulize swali.. Hivi mtu akikupa zawadi ya thamani sana Si utamshukuru kwa zawadi hiyo!?.., BILA SHAKA JIBU NI NDIYO (HIVYO BASI TUNAMUAMINI MOLA WETU KAMA SHUKRANI YETU KWAKE KWA NEEMA MBALIMBALI ALIZOTUPA)
Na sio eti kwa kuhofia... We do it out of love& gratefulness. AHSANTE
 
Kwaiyo wewe ndiye uliyeomba uumbwe au huyo mungu ndiye aliamua akuumbe bila hata wewe kumuomba?
yeye si ndio kakuumba kwa mujibu wa imani zenu?

sasa kama yeye ndio kakuumba kwa kutaka kwake mwenyewe, kukupa hizo neema si ndio wajibu wake?
kwa nini iwe ni zawadi?
kwa nini umshukuru?
ulimuomba akuumbe?

Halafu nikisema huyo mungu ni dikteta na nyie ni misukule yake unaona nawatukana!!!

Yani mtoto umzae mwenyewe, kwa sababu ya starehe zako mwenyewe, halafu ukimnunulia nguo unataka akushukuru??!!!

Huyo ni mtoto wako au msukule wako?
 
Je kusema ahsante kwa baba yako kwa nguo alizokununulia licha ya kwamba alikuzaa yeye mwenyewe ni jambo baya!? ... Bila shaka ni jambo zuri.
Ukifanyiwa wema rudisha wema... Sio unafanyiwa wema wewe una rudisha matusi na dharau. HAIINGII AKILINI
 
Imagine unaambiwa eti umepewa uhuru wa kuchagua halafu ukichagua upande tofauti na mungu unaadhibiwa.Na bado watu wanakubali wana uhuru wa kuchagua!!
Watu kama hao napowaita misukule siwatukani.

Yani mtu ni mwanafunzi wa shule A, Mwalimu mkuu wa hiyo shule anatangaza kuwa kawapa uhuru wa kuchagua kati ya masomo ya sayansi na masomo ya uchumi lakini wajue kuwa atakaechagua masomo ya uchumi atafukuzwa shule!!

kwa anaependa uchumi na hapendi kufukuzwa shule atasema ana uhuru wa kuchagua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…