Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.
Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"
Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?
Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.
Kwanini nimefikia hitimisho hilo?
Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.
Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.
1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.
2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.
Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.
Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.
Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.
Nawasilisha.
Mtu akisoma hoja zako kwa makini atagundua kuwa, umeenda Chuo Kikuu wakati hujamaliza hata Chekechea.
Ungeanza kwanza kujibu maswali mengine mengi kabla ya kumfikia Mungu
Mfano wa baadhi ya maswali;
1. Nani aliumba watu/viumbe wengine kama wanyama na miti
2. Nani aliumba Milima, Moto, hewa nk
3. Nani aliumba maji (bahari)
4. Nani aliumba dunia, Jua na sayari nyingi unazozifaham kama unaelimu ya Jiografia au Fizikia
Ukishamaliza kufikiria vyote hivyo kwa makini na sio kijuu juu;
Utagundua kuwa Binadamu ni kitu kidogo sana kwenye uumbaji; kwani kulikuwa na complex structure kabla hata ya kuwepo kwa Binadamu la sivyo, Binadamu hangeweza kuishi huku duniani (mfano bila Jua, maji, hewa, chakula nk ). Siamini kama kuna mtu aliyesoma anaweza kuwa Mbumbumbu kiasi cha kufikiri kuwa, Binadamu aliyeko ndani ya dunia aliyoikuta ikiwa na kila kitu, eti naye ni muumbaji?
Mwanadamu huyu, ambaye hata hawezi kujua siku ya kufa kama sio kuzuia basi kifo? shame!!!
Sasa kwa kifupi
Hiyo Nguvu iliyofanya Dunia na vilivyomo ndani ya dunia, na uwepo wa Sayari Nyingine likiwepo Jua, ndiyo huitwa
MUNGU
Mungu ni mmoja tu, na sio Kiumbe kwani hajaumbwa, hana mwanzo wala mwisho (kwa kuwa alikuwepo jana leo na hata milele), Hajazaa wala hajazaliwa (kwa hiyo hafi)