Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
Si uende umuulize yeye? Wewe una miaka mingapi? Je uliwahi kupata magonjwa ya akili au kuzimia au kifafa? Je ulisoma hicho ulichoandika kabla ya kukirusha? Unavyodhani wewe kwa hali yako jibu la swali lako ni lipi mwanangu?
 
Ameumba kila kitu kinachoonekana na kisichooonekana
Una uthibitisho gani yeye ndo kaviumba? Ulikuwepo ukamuona akiumba?

Na je yeye nani kamuumba? Na yuko wapi? Na anafanya nini saivi? Unaweza kumuita akaja akajieleza?
 
Wewe unataka MUNGU ajidhihirishe kwa namna gani kwako?
Kabla sijafunguka macho nilimtegemea kwa kipindi kirefu sana, akaniacha bila msaada wowote

Alikataa kunisaidia, ndo nikagundua kumbe naomba kitu kwa mtu ambaye hayupo, nikafuata njia nyingine nikafanikiwa.
 
Kabla sijafunguka macho nilimtegemea kwa kipindi kirefu sana, akaniacha bila msaada wowote

Alikataa kunisaidia, ndo nikagundua kumbe naomba kitu kwa mtu ambaye hayupo, nikafuata njia nyingine nikafanikiwa.
Mkuu Ipo siku utakuja kumjua MUNGU wa kweli
 
Mtu anaejifungia kwenye box la elimu moja tu ya sayansi pekee Ili kupata majibu ya hoja zake huwa kajifunga kwenye ufahamu.
Utadhani sayansi pekee ndio jawabu la KILA kitu
Hata hapo ulivyoandika umetumia sayansi.

Jaribu kuandika bila kutumia sayansi nitakuelewa zaidi.

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
 
Uneza kuta kila kitu ni Mungu, binadamu,wanyama, kila kitu ila tu hatujui
 
Yaani jamaa anakuja na hoja nyepesi hivi, kupinga uwepo wa Mungu? Mm nikadhani utaweka huo uliodai ni utafiti wa kushiba kutetea hoja yako. Lakni ni bla bla tu!
 
Unaweza kuthibitisha hili?? Maana umeweka claim isiyo na ushahidi wowote...Na hiyo claim mwenyewe naweza kusema kwa ulimwengu pia, Kuwa ulimwengu hahuhitaji chanzo kwakuwa haujawahi kutokuwepo.
Jibu swali nililokuuliza.
 
Siwezi kupoteza ATP zangu kujadili hizi mada, nenda katafute walugaluga huko mimi sina huo muda wa kubishana na wanaoipinga sayansi.
Shukrani.
Hii ndiyo shida ya kujadili mambo na mashabiki wa Sayansi. Mimi. Naishi katika Sayansi sababu ni mtu wa hayo mambo.

Kama wapo Wanasayansi au hata Wahandisi unao waamini walete nijadili ane nao, sababu hao wanaishi humo. Huenda tukaelewana nao.
 
Back
Top Bottom