Unakabiliana vipi na waumini wanaolazimisha salamu za kiimani bila kujuwa imani ya mtu mwingine

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
 
Naona mna complicate maisha tu mara nyingine;
Uninisalimia "Tumsifu Yesu Kristo" nakujibu "milele akina"
Ukinisalimia "Assalamualaikum" nakujibu "alaikum Islam"
Ukinipa salamu nyingine yoyote nakujibu kama naelewa jibu; ndio Utanzania wenyewe
 
Mtu wa makamo ya baba yako umuitikie "POA"?

kwani Bwana Yesu asifiwe au Asalam Aleko zina shida gani?

Kijana huna nidhamu kabisa..
Kwa upande wa Uislam haijaelekeza kumpa Asalam Aleykum asiekua muislam, kama siyo muislam msalimie "Habari yako, mambo vipi, kwema..."

Kwahiyo jamaa yuko sawa hatakiwi kupewa salam hiyo kama siyo muislam.
 
Maana ya asalam aleykum (kama sijakosea). Ni nini??
Alafu kingine atajuaje kama huyu ni muislamu au sio?
Weka vifungu vinavyokataza
Kwa upande wa Uislam haijaelekeza kumpa Asalam Aleykum asiekua muislam, kama siyo muislam msalimie "Habari yako, mambo vipi, kwema..."

Kwahiyo jamaa yuko sawa hatakiwi kupewa salam hiyo kama siyo muislam.
 
Naona mna complicate maisha tu mara nyingine;
Uninisalimia "Tumsifu Yesu Kristo" nakujibu "milele akina"
Ukinisalimia "Assalamualaikum" nakujibu "alaikum Islam"
Ukinipa salamu nyingine yoyote nakujibu kama naelewa jibu; ndio Utanzania wenyewe
Wewe inaonekana ni lipagani ,maana hata hiyo ya kikristu umeenda Chaka

Sasa si Bora anayesema poa ili kufupisha mba mba
 
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Hai sound Bwana Yesu asifiwe jamaa POA, samaleko jamaa POA
 
Back
Top Bottom