Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.
Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.
Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.
Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Ni kweli haijakaa poa kumwambia mtu assalaamu àlaykum wakati hana dalili za moja kwa moja kuwa ni mwislamu. Kwa nchi zingine huko najua ndo watu wanatakiwa wapate tabu kwenye mambo ya salamu ila siyo sisi maana tuna salamu nyingi sana kwa mfano;
1. Habari? kwema? Za saizi? Salama? Za leo? Amani? (Salamu za jumla kwa yeyote)
2. Shwari? Niaje? Mambo? Vipi? (Za jumla kwa vijana, mkubwa kwenda mdogo na makundi fulani fulani)
3. Za asubuhi? Za mchana? Za jioni? Za kutwa? Za mwamko? (Salamu za jumla kwa yeyote kulingana na nyakati)
4. Za kazi? Za uzima? Za kwako/kwenu? Za siku? (Salamu za jumla kwa yeyote kulingana na mazingira, majukumu nk)
Kusalimiana ni mila na desturi zetu. Kwa sisi waislamu kutoa salamu ni jambo linalosisitizwa sana na kuitikia salamu ni wajibu/lazima. Sasa inatokea mtu unamjua kabisa siyo mwislamu au humjui lakini ana dalili zote za kuonesha siyo mwislamu au hata unamjua ila huna uhakika kama ni mwislamu au siyo mwislamu halafu unambebesha bonge la ASSALAAMU ÀLAYKUM jamani hivi huoni unatafuta nongwa akosee useme anasanifu au anyamaze useme anabagua? Salamu zote hizo hapo juu ina maana umekosa hata moja ya kuitumia kweli? Ni ulimbukeni wa dini huo!
Kama kawaida mimi ni mlinganiaji wa dini hivyo na hapa nisilog out bila kuwaweka sawa waislamu na wakristo kuhusu salamu. Ukweli ni kwamba TAKBIR, BWANA APEWE SIFA, TUMSIFU YESU KRISTO, BWANA ASIFIWE, TUMSIFU MTUME, na maneno mengine mengi mfano wa hayo SIYO KATIKA SALAMU bali salamu ni ASSALAAMU ÀLAYKUM au AMANI IWE NANYI na maneno mengine yenye maana sawa na hiyo.
Tukiona muumini kakutana na mwenzake halafu eti amwambie BWANA YESU ASIFIWE au TUMSIFU MTUME au TAKBIR huku akikusudia hiyo ndiyo salamu basi tunamchukulia huyo ni mshamba na limbukeni wa dini. Usipanic twende taratibu unielewe. Hayo ni maneno ya vibwagizo tu au kwa kiswahili cha kawaida kabisa tunaweza kusema ni maneno ya kuingizia tu katika makutano ya waumini wa kiislamu au kikristo. Salamu iliyothibiti kote kote ni hiyo niliyoisema hapo juu