Unakabiliana vipi na waumini wanaolazimisha salamu za kiimani bila kujuwa imani ya mtu mwingine

Unakabiliana vipi na waumini wanaolazimisha salamu za kiimani bila kujuwa imani ya mtu mwingine

Kuna wazee wengine unampa heshima vizuri ila ukimkuta anavyozungumza na vi binti vya 2000 tena vidogo, ndipo unagundua wakina Baltazari wapo wengi.
Kwani ukitoa heshima kwa huyo mzee kuna shida gani? Wewe hayo ya kuongea na vibinti inakuhu nini
 
Nakumbuka kuna ndugu mmoja huyo yan mkikutana tu habar za wokovu,hata akukute wapi,ikabidi ukimwona kwa mbali unajiongeza kumkimbia
Mi Kuna mmoja nilikuwa namkimbia, alipogundua kuwa namkimbia akawa kila akiniona ananivizia na kunifungulia lecture ya mahubiri yaliyojaa kukebehi imani yangu nikagundua kuwa hajaiva sana kwenye bibilia basi nikamwuliza. Kuwa kati ya Yesu na Maria nani ni mkubwa akasema Maria eti Kwa sababu alimzaa yesu. Nilimcheka sana mpaka Leo akiniona aninitoroka chap.
 
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Wape tu jibu ambalo lipo karibu kinywani mwako, japo watakuona mtata ila siku zote marehemu ndiyo huwa mchokozi
 
haya maswali ungemuuliza bibi yako kabla hujaja Dar.

Nakumbuka kipindi unaomba msaada hapa JF ulikua mstaarabu na uliitikia kila aina salam..

Leo kijana umelijua JIJI, umeota mapembe
[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Binafsi, kitu kisichonipunguzia chochote Wala hakinifikirishi, huwa Niko flexible kwelikweli.
 
Salamu ipi, Bwana Yesu asifiwe/Tumsifu Yesu Kristu au asalaam aleikum? Salamu hizo wanapeana waumini wa dini/imani hiyo tu, kama si mshirika/muumini wa dini/imani hiyo hupewi/husalimiwi, utapewa salamu ya kawaida tu.
 
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Ni kweli haijakaa poa kumwambia mtu assalaamu àlaykum wakati hana dalili za moja kwa moja kuwa ni mwislamu. Kwa nchi zingine huko najua ndo watu wanatakiwa wapate tabu kwenye mambo ya salamu ila siyo sisi maana tuna salamu nyingi sana kwa mfano;

1. Habari? kwema? Za saizi? Salama? Za leo? Amani? (Salamu za jumla kwa yeyote)
2. Shwari? Niaje? Mambo? Vipi? (Za jumla kwa vijana, mkubwa kwenda mdogo na makundi fulani fulani)
3. Za asubuhi? Za mchana? Za jioni? Za kutwa? Za mwamko? (Salamu za jumla kwa yeyote kulingana na nyakati)
4. Za kazi? Za uzima? Za kwako/kwenu? Za siku? (Salamu za jumla kwa yeyote kulingana na mazingira, majukumu nk)

Kusalimiana ni mila na desturi zetu. Kwa sisi waislamu kutoa salamu ni jambo linalosisitizwa sana na kuitikia salamu ni wajibu/lazima. Sasa inatokea mtu unamjua kabisa siyo mwislamu au humjui lakini ana dalili zote za kuonesha siyo mwislamu au hata unamjua ila huna uhakika kama ni mwislamu au siyo mwislamu halafu unambebesha bonge la ASSALAAMU ÀLAYKUM jamani hivi huoni unatafuta nongwa akosee useme anasanifu au anyamaze useme anabagua? Salamu zote hizo hapo juu ina maana umekosa hata moja ya kuitumia kweli? Ni ulimbukeni wa dini huo!

Kama kawaida mimi ni mlinganiaji wa dini hivyo na hapa nisilog out bila kuwaweka sawa waislamu na wakristo kuhusu salamu. Ukweli ni kwamba TAKBIR, BWANA APEWE SIFA, TUMSIFU YESU KRISTO, BWANA ASIFIWE, TUMSIFU MTUME, na maneno mengine mengi mfano wa hayo SIYO KATIKA SALAMU bali salamu ni ASSALAAMU ÀLAYKUM au AMANI IWE NANYI na maneno mengine yenye maana sawa na hiyo.

Tukiona muumini kakutana na mwenzake halafu eti amwambie BWANA YESU ASIFIWE au TUMSIFU MTUME au TAKBIR huku akikusudia hiyo ndiyo salamu basi tunamchukulia huyo ni mshamba na limbukeni wa dini. Usipanic twende taratibu unielewe. Hayo ni maneno ya vibwagizo tu au kwa kiswahili cha kawaida kabisa tunaweza kusema ni maneno ya kuingizia tu katika makutano ya waumini wa kiislamu au kikristo. Salamu iliyothibiti kote kote ni hiyo niliyoisema hapo juu
 
Back
Top Bottom