Unakosea, Unakosea na nasema tena Unakosea wenye Akili hawashindani na 'System' Kibwege (Kipumbavu) hivi..shauri yako!!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Nakuonea sana Huruma japo Wanafiki na Wasiojua mambo ya Kimtambuka duniani watakupongeza na kukujaza Upepo, ila nina uhakika wa 100% hao hao baadae watakuacha peke yako na Wengineo kuanza Kukucheka japo juzi, Jana na leo watakuona Shujaa.

Najua katika huu Uzi wangu nitashambuliwa mno na Wanafiki wale wale ambao wana Mihemko ya Kisiasa na Chuki ila naamini wenye Akili Kubwa watanielewa vyema kabisa.

Watu waliosoma vyema Strategic Studies watakumbuka hii Kanuni Kuu ya KUUSOMA KWANZA MCHEZO KABLA YA KUUCHEZA na unatakiwa kuwa very Smart Kupambana na Tawala nyingi za Kimafia barani Afrika vinginevyo utakuwa unakaribisha DHAHAMA yako mwenyewe na baadae kuja Kujuta.

 
Shida iliyopo ni moja tu! Watu wakiamua kusema, kamwe hutaweza kuwanyamazisha wote! Unamfunga Lissu, Heche anaendelea kusema! Unamshambulia Kitima, Gwajima anajitokeza! Unamuua Ben Saanane, Mdude anaibuka! Unamuua Mdude, anatokea mwingine!!

Binafsi sikumbuki kama kuna mtawala katili aliwahi kunyamazisha midomo ya wakosoaji wake. Maana ukimuua mmoja, wanazaliwa wengine 100. Njia pekee ya kuondokana na haya makando kando ni kwa mtawala tu kukubali kusikiliza mawazo ya wananchi, badala ya kusikiliza mawazo potofu ya kundi baya la wahuni waliomzunguka.
 
Tawala za kiafrica kupambana nazo kwa kwa maneno ni ngumu ....ndo maana wengine wanamua kwenda msituni kuongea kwa risisa kwa risasi
 
Gentamycine.
Ulitaka Utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali yaendelee kutukuzwa ?!
Au mimi ndiyo sikuelewi !

Au watu wote wanyamazishwe ?
Nyerere aliwahi kusema ukiishaanza kula nyama za watu hutaacha. Wameanza kwa wapinzani hamkujali. Leo ni kwa yeyote anayethubutu.
 
GENTAMYCINE kila jambo huwa lina mwisho wake. Mi ninvyoona hapa ni ule utendaji kazi wa Dkt Kikwete (rejea ile kauli yake labda mambo yaharibike sana), na pia ukicheki kiundani aki riep current ceo ina make sense laana ya kushindana na nguvu za Mungu parapanda italia na rais na makamu mwingine atakuja na kitakachofuata ni 🤬 kumsema vibaya kama old ceo kwenda mbele na kusafisha kisiwa chote rudisha kwao. Sasa sijui huu mtego nani kaingia mkenge, ndiyo maana it is too early kufikia conclusion my bosi wangu.
 
Pamoja na hayo ebu pia tujiulize hivi nchi hii kwasasa ni kosa la jinai kukemea utekaji?

Ni kosa kubwa lipi alilolifanya Gwajima linalostahili haya yote anayofanyiwa. Ina maana watawala wana haki ya kutuvuna/kutuua sisi raia kila tunapoonekana kuwakosoa.

Je tuamini kwamba serikali ndiyo inayoteka, kutesa na kuua raia wake? Mbona watu wanaojitokeza kukemea kwa nguvu uovu unaofanywa nchi hii waonekane wanazipinga mamlaka?

Kama taifa tunatakiwa tujitafakari sana. Tunakoelekea siko kabisa.
 
Kila kitu ni strategic strategic.. hiyo ni looserthink. Wenye strategies walishatekwa na kuuawa, wengine wapo wanazushiwa kesi na wako mahabusu.. hzi 'strategies' ni doctrines of docility.

Kama "kocha" muda mwingine, mbinu zikishafeli, ushapigwa tatu na dakika zimeenda, ni kuingizia striker mwingine na kubutua mipira mbele tu.
 
Wabongo kwa kujifanya wana akili na maujuzi ya usalama dah, ngachoka, we mwenye akili na unayejua mbinu unatumia id fake kuelekeza! Acha wanaume wafanye kazi kule kama wamekosea we fanya yako mema!

Something must be done kwa hali tuliyofikia, hamnaga right time wala right process, hata Nyerere hakusubiri right/perfect time ndio aombe uhuru, we subiri kande tu hapo ushibe ubaki kupumua tu, hizi sio league zako ukiona huelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…