Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,435
- 3,120
Tunaelekea wapi kama wanaume?
Kuna kundi la wanaume ambao kwa namna ya kushangaza wamezoea kuishi ndani ya unyonge—unyonge wa kutokuwa na hata shilingi mfukoni. Hali ni mbaya kiasi kwamba hata mtu ambaye humjui binafsi, ukimuangalia tu unajisikia kero. Kwa nini? Kwa sababu umaskini wake umegeuka kuwa mfumo wa maisha na siyo hali ya mpito.
Unakuwaje mtu mzima, kila ukipewa mchongo au agizo fulani, lazima uanze kwa kusema "nisaidie nauli kwanza"? Mtu anakwambia fanya A, B, C ukifika nitakulipa, bado unahitaji kuongozwa hadi mlangoni? Huu siyo ukosefu wa hela tu, ni ukosefu wa utu wa kiume. Kama hali hii ingetokea mara moja moja, tungesema siku hazifanani. Lakini ikitokea mara kwa mara, hapo kuna tatizo la tabia, siyo uchumi.
Yaani mtu anaitwa baa, kwenda kunywa bia za bure—bado anataka apatiwe nauli ya kufika huko! Kweli? Hii ni aibu. Hatuwezi kuendelea kulea kizazi cha wanaume waliosalimu amri kwa maisha. Wanaume waliokubali kuishi kwa kuombaomba, wanaume waliogeuza utegemezi kuwa haki yao ya msingi.
Swali la msingi: Tunalilea taifa la aina gani la wanaume? Wanaume wanaokimbia wajibu, wanaosubiri kusaidiwa kila hatua, wanaume wasiojiamini?
Hali hii lazima ikome. Wanaume lazima waamke, wajitambue, na wachukue nafasi yao ya uongozi wa maisha yao wenyewe. Unyonge siyo sifa. Umaskini siyo utambulisho. Na kuombaomba siyo njia ya maisha.