Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Wanaume mnapenda kulalamika sana, sisi wanawake vitu vingi huwa tunapuuzia Ila na nyie mna kero sema wanawake tunasahau haraka
Si kwasababu tunalipia. Nanyie mngekuwa mnatupa pesa na ya kutolea tungekuwa tunasahau. Sasa hela tutoe halafu yale maumivu ya kutoa tubakie nayo ? Hapana lazima tuwatukane hata kidogo au tuwape kauli za dharau ili tubalance shobo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yaani mwanaume anapelekeshwa naye anapelekesheka tu[emoji134]dah wa hivi anachosha sana..hakuna hata amsha amsha,anazubaa mno kama gari bovu anaenda popote anakopelekwa.
[emoji23][emoji23] your not serious.. Siku wakibadilika ndo basi tena. Unakuta mtu alikua amefunga zipu yake lakini baada ya sijui kuamsha amasha"unakuta kila siku utapigwa matukio mpaka utatamani ile hali ya "uzoba".
 
Mimi nilikuwa nimemaliza chuo 2009 and then 2011 nikapata kakazi fulani, basi naye alikuwa mwalimu na anakaa kota za shule, baada ya muda akaanza kuja kulala kwangu anaweza kaa hata mwezi, nikaenda kwao na nikawa nataka kupeleka barua ya posa, basi sijui alibadilikia wapi, akaniambia yani barua mpaka mwakani? Mie nataka mwaka huu kama haupo tayari siwezi acha niondoke, tena akanizodoa na kidole, kimara mwisho hapo getoni kwangu, mie nikamuambia basi sawa kama umeamua hivyo, ila tambua huko duniani utapata elimu na kuijua thamani yangu, siku ya siku jumamosi naenda kazini tulikuwa tunafanya nusu siku, akaniambia halfcastmangi naomba nauli nirudi kwangu, akaanza funga funga nguo zake, nikamuuliza shilingi ngapi, akasema 20k, hapo ni 2013. Mie nikampa 40k kabisa, akasema hunipeleki, nikamuambia naenda kazini. Basi nikiwa ofisini saa 5 hivi akanitumia meseji kuwa kwaheri mimi nimeondoka. Nikamjibu haya asante kwa taarifa. Ile nimerudi geto kama saa 9 hivi mchana, nikakuta kachukua mpaka mapazia, friji, yani kitchen appliances zote na shuka kaniachia moja tu, kuna shati alininunulia, nikakuta kalichana chana, kuna kama lita 4 hivi nilikuwa naweka coins kasepa nacho, kiukweli niliumia sana siji sahau siku iyo nilienda kunywa grants kubwa 2. Halafu nikajisema sintamtafuta tena, baada ya wiki akanipigia eti naomba tuonane nikupe funguo yako, niliambia itupe tu, sikuwahi muona wala kumpigia tena.

Ikapita miaka kama 6 hivi nikaona text, pole kwa kufiwa na mama, kweli mama yangu alimpenda sana huyu binti. Basi nikamjibu asante, ikapita miezi 4 akatuma tena text nimeonana na mdogo wako anayesomea udaktari hapa chuoni kwao kwenye lift, nikamuambia haya, hapo tayari nikasikia alizalishwa na mjuba akakimbia na 120 shwaaang.
Mwaka 2021 nakumbuka nikawa botswana nikapiga picha nikiwa mgahawani ktk mall fulani hivi nikaweka status, ghafla naona ananitext habari za miaka, nikamjibu nzuri tu, mara hapo wapi, nikamjibu gaborone, botswana, mara hongera sana halfcastmangi wewe mpambanaji sana, siku nikawa kwa madiba nikaweza tena status kukakera tu, kakaamua kupiga kabisa, nikamuambia unanipigia na mumeo akiona itakuwaje, akajibu kuna wanaume siku hizi, wanaume mlikuwa nyie bwana [emoji23][emoji23]. Basi kakawa kanaendelea tu kulazimisha mahusiano, mwaka jana nikatupia picha nipo na shemeji yenu, kakaniandikia meseji eti kuwa mbona huyo kama sio mtanzania umeamua kuoa huko nn, nikamjibu huyu ni mmasai mbona, halafu bahati mbaya wanafanana majina, nikuambia tena ana jina kama lako,

Wiki 2 zimepita sasa akanipigia anasema anaomba msamaha kwa yote yaliyotokea na anajuta sana yani sana, eti alidanganywa na shoga ake na walishahombana naye. Akawa anasema ananipenda sana na kamwe hawezi kunisahau.

Juzi kakapiga WhatsApp upo wapi, nikakaambia kwa madiba, kakasema kanaomba zawadi na kanaomba simu, ya kwake kioo ni shida, kakaomba nikakopeshe na 200k.

Kiukweli nilimpenda sana yani sana, sikuwahi cheat nikiwa naye, nilimtunza kama malkia, ila kile kidole alinisota nacho, nilijiapiza kutokuwa naye tena, haswa kwa mie mchaga wa kibosho ni fedheha sana.

Nilimpenda ila kwasasa hana nafasi tena, malkia wangu nilimpa story kamili, akaomba kuhakiki, nikamruhusu, kwa sasa nampenda sana masai wangu. Nilikuja gundua wakati ule alitamani wenye mali nyingi na kuona sina mwelekeo.

Namalizia kwa kusema kweli wanaume kuna majibu au kauli huwa tunatamkiwa, ukiwa na roho ndogo unaweza kujiuwa, kugeukia ulevi au uraibu wowote, sio wote tunaweza handle the situation. Huyo alinitamkia kauli za dharau nyingi tu sijaziandika hapa. Pia nikiri sio wanawake wote walio na tabia mbaya au mbovu, hapana wapo wema na wanaojua thamani ya mahusiano, heshima kwa mwenza wake.

Kiufupi nami huo ndio mkasa niliwahi kutana nao na nikaumia sana, mbaya zaidi wakati ananiacha na kazi mradi ukaisha nikawa jobless, nikauza ka vitz kangu bado maisha yakanichapa sana, nikakonda kama nina ngwengwe kwa maana nilikuwa namuwaza yeye tu.
 
Pole mkuu
 
Ukamuoa yeye?

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Punguza kupenda ndugu,utapoteza afya ya akili...,shida pia vijana mnafuata sura na shape ndio maana mnalia Lia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mwanaume mzima unakosaje pesa"

"Nikikupea utawezana au utanichafua tu"

"Nilikuonea tu huruma ndio maana nilikukubali"

.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…