Unakumbuka Kauli tata za Mama zetu? Hebu tupia na ya kwako…

Unakumbuka Kauli tata za Mama zetu? Hebu tupia na ya kwako…

niliwahi pita dirishani nikaingia jikoni kulamba sukari ile natoa tu kichwa nitoke bi mkubwa huyu hapa kumbe aliniona nikiingia akaandaa silaha za maangamizi, nilipigwa na fagio la kichwa nikaangukia jikoni kwenye sufuria kubwa 😂.. Namshukuru sana mama kwa kipigo kile maana huenda lisingetokea lile ningekuwa mwizi.
 
Ndo maana una kichwa kirefu,aahaaaaa
 
1. Mama: Naongea na wewe unajifanya kukaa kimya siyo?
Mtoto: Lakini mama......
Mama: Nyamaza, yaani mimi naongea na wewe unajifanya kuongea?

2. Haya nenda kacheze halafu uchelewe kurudi. (Kakwambia uchelewe sasa ole wako uchelewe)

3. Baada ya kumuogesha mtoto eti anamwambia halafu ukajichafue tena!

Tupia na nyingine!
Kwanini "tata"? Sijawahi kuuona utata hata mmoja kwenye kauli za wazee wangu, zote zilililenga kunijenga kimaisha.
 
Back
Top Bottom