Ukucheza baba na mama..??Kuchimba udongo na kutengeneza watoto.
Kwenda dukani kuiba vitu (mchele) na kujipikilisha kwenye vikopo.
Kuna siku niliiba dagaa nikakimbia toilet daaaah nilifatwa hadi toi yani [emoji848]
Vibaya mnoooUlikuwa unapuna watu kwenye Gololi?
Kuwinda ndege kwa manati ni mchezo au ni kutafuta mboga ya ugali?Nikiwa mtoto bhana, Nilikuwa napenda sana michezo, moja ya mchezo ni Kuendesha lingi, Kuwinda ndege kwa manati.
Kuna ile Unatengeneza gari la mbao na mipira inakuwa kama spring na unaweka kamba mbele na mti inakata hadi kona, na kukata malapa (Kanda Mbili) kama matairi
Kingine bhana Niliwahi kwenda kuoga kwenye bwawa kubwa mnoo ambalo kingo zake ni za mfinyanzi, hivyo mvua ikinyesha au zikilowa huwezi kutoka, na bwawa lilikuwa kubwa mnoo
Wewe unakumbuka mchezo gani?
View attachment 2918070
Nilipomaliza STD 7 mama akanipiga marufuku. So ikabaki karata ambazo tulikuwa tunacheza wenyewe nyumbani na mama na madogo 🤣Umetisha sana ndugu