Unakumbuka Mchezo gani ukiwa Mtoto?

Unakumbuka Mchezo gani ukiwa Mtoto?

Mchezo wa kujificha(kombolela)
Baba na mama
Kula umbakishie baba
Kujipikilisha(pishi la kwanza kulipika ni pilau kwenye kikopo cha kibatari)
Kucheza mpira wa miguu
Mdako
Na mengineyo
 
magqri ya mbao afu tunaenda masafa kutembea na magari yetu unatoka hom saa nane ubarud saa moja au 12😂😂
 
Nikiwa mtoto bhana, Nilikuwa napenda sana michezo, moja ya mchezo ni Kuendesha lingi, Kuwinda ndege kwa manati.

Kuna ile Unatengeneza gari la mbao na mipira inakuwa kama spring na unaweka kamba mbele na mti inakata hadi kona, na kukata malapa (Kanda Mbili) kama matairi

Kingine bhana Niliwahi kwenda kuoga kwenye bwawa kubwa mnoo ambalo kingo zake ni za mfinyanzi, hivyo mvua ikinyesha au zikilowa huwezi kutoka, na bwawa lilikuwa kubwa mnoo

Wewe unakumbuka mchezo gani?
View attachment 2918070
Kombolera ilikua balaa,siku hiyo na tumpe tumeenda kukanyagana choo cha public.
Kaja fala gani sijui kunya katukuta tunapigana miti.
Hapo tuna miaka haizidi mitano.
Aisee tulimpiga kikumbo yule jamaa tukatokomea.
Ile unakimbia mpk unajiuliza hivi huku nakimbilia wapi? Unaanza kurudi
Bahati nzuri yule jamaa aliyeyusha,angepeleka kesi mahome tungekua labda tushadedi.
Wale madingi walikua wanoko kishenzi.
 
Mchezo wa kujificha(kombolela)
Baba na mama
Kula umbakishie baba
Kujipikilisha(pishi la kwanza kulipika ni pilau kwenye kikopo cha kibatari)
Kucheza mpira wa miguu
Mdako
Na mengineyo
Nasubiri hapo uliposema ''Na mengineyo'' humo nahisi ndio patamu zaidi,endelea kufunguka pls.
 
Nilikua najifanya eti mchezesha Mazingaombwe kumbe nafake tu hakuna lolote,

Niliwapiga sana hela madogo wenzangu.
 
Na mke wangu utotoni Josefin, ka black beauty.
Tunapika mchanga wetu kwenye kopo la blue band km utaiva tule.
Tunachochea moto ili mchanga uive aah wapi
badae tunazama kwenye pagale tunatinduana tu tulikua tunaita kufanya matusi😁.
 
Mtaa wetu tulikua vitoto vya kiume tupu, michezo ya kibaba na mama, kuruka kamba, kujificha ilikua inaonekana ni ya kimama, ukikutwa unacheza hiyo na videm vya mtaa wa pili unatengwa na wauni.

Sisi wetu ilikua kuendesha matairi ya magari, pikipiki kwenda mtoni/ziwani na sana sana mpira wa miguu.
 
Kibaba mamaaa nimekula sana hizo wanajiita pisi kali now days
 
Rede, mdako, mputa, bao ile ya kucheza na kigae, madangi ya moto.
[emoji8][emoji8][emoji8]
 
Ilikuwa ni ugomvi wa kufa mtu baina yetu sisi (wajukuu) na babu kwasababu ya kuharibu migomba yake kwa kuikata ili tuichambue maganda ya nje kwa lengo la kupata ile nirija ya katikati ambayo tulikuwa tunaichonga vizuri mno kuunda magari ya aina tofauti tofauti kisha tunakuwa tunashindanisha gari ipi inabeba mzigo wa maana na yenye mbio halafu haipinduki pinduki ovyo😃😃utoto uharibufu
 
gololi

kibaba na kimama

kula mbakishie baba

kutengeneza baruti kipindi cha mwaka mpya, kutengeneza magari ya matope, kuendesha maringi, kutengeneza tochi na betri za panasonic.

karata za kutimiza

mpira wa miguu (cha ndimu kazi) kombe biscuit

kutengeza ndege za karatasi (shule) nilikula sana hamsini hamsini zao

kwa kifupi watoto wa enzi hizo tuli enjoy sana utoto wetu na michezo yetu ilikuwa na ubunifu ndani yake ukiwa kilaza huwezi kucheza baadhi ya michezo
 
Gololi, kamba, rede, mpira Kwa mbali, baba na mama. Sisahau hii tuliachwa na mtoto wa kaka tubaki na kachanga. Maza wa mtoto yupo shambani analima. Sisi si tukaanza yetu bana, mtoto akaanza kulia wee sisi hata hatukusikia. Akaja home akambeba mtoto akabembeleza. Akatutafuta akatupata aisee tulizichezea za kutosha na kitisho Cha nitaenda kumwambia mama yako. Kile kitu kiliondoa confidence Kwa miaka mingine 25 hivi. Yani nilijifunza kitu pale kwamba ni busara kukaa na mtoto na kumkanya Kwa kumwambia kuliko kumchapa.
Kile kitendo niliacha lakini kilinifanya niogope wasichana. Nimekuja kujua hilo tatizo mwaka juzi hapo nipo tayari 28. Bado nakarabati makosa ya zile fimbo za 98 mpaka sasa hivi.
 
Kuchimba udongo na kutengeneza watoto.

Kwenda dukani kuiba vitu (mchele) na kujipikilisha kwenye vikopo.
Kuna siku niliiba dagaa nikakimbia toilet daaaah nilifatwa hadi toi yani 🤔
Baba na mama. Mi baba we mama. Unakumbuka siku 1 tulichapwa kwani mama yako alitufuma tukifanya ya bibi na babu.
 
Picha inajieleza.
FB_IMG_1709170841888.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1709170841888.jpg
    FB_IMG_1709170841888.jpg
    36.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom