Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Ni kweli Mkuu, Philip Ndunguru ndio mchoraji wa katuni orijino za kina Kipepe, Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Mwinyi Mpeku na hata kumchora Mzee Sani mwenyewe
Watoto wengine waliokuwa wanaishi Bara nyakati zile, walikuwa wanafikiri kuwa wale akina Dr Love Pimbi,Mzee Sani,Mzee Kifimbo Cheza,Sokomoko,Lodilofa,Ndumila kuwili, wote ni watu wa ukweli,na wanaishi Dar!!
 
Watoto wengine waliokuwa wanaishi Bara nyakati zile, walikuwa wanafikiri kuwa wale akina Dr Love Pimbi,Mzee Sani,Mzee Kifimbo Cheza,Sokomoko,Lodilofa,Ndumila kuwili, wote ni watu wa ukweli,na wanaishi Dar!!
Dah, amakweli tasnia ya uandishi wa vibonzo na ucheshi imetoka mbali sana, ni kweli kabisa usemayo Chief, watu wengine walidhani hawa jamaa wana exist in real life

Na kuna wale kwenye magazeti ya Uhuru na Mzalendo kina Chakubanga, Polo, Bushiri na Chupaki kama walivokua wanachorwa na somebody Gregory nadhani, nao walitingisha sana enzi zile
 
Hakika ilipendeza!
Kweli mkuu. Nakumbuka 90 kombe la dunia nchini italia. Tulikuwa tukiangalia pale chuo cha ushirika, tv yao ilikuwa ni zile zisizo na rangi.(black n white) ccp pia tulikuwa tunaangalia. Wao walikuwa na coloured tv.
 
Nyimbo maarufu enzi hizo ni colombiaa Colombia vitambaa vya chirmen viatu utankoma sanane wimbo wa bonite kiwanda Cha sooodaaa
Watoto wa siku hizi hawaelewi hizo mambo kabisa
 
Hili gazeti liliua kabisa soko la magazeti kama Lawalawa,Film Tanzania
 
Mhenga mwenzangu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namuona prof ndumilakuwili na Kofia lake kama mlinzi wa kiongozi kutoka ofisi ya raisi(usalama wa taifa)😁😁😁😁
 
Mzee mbona hamuwazungumzii wa gazeti la Bongo, kuna akina Bob Mikwara, Chepe, Mshikaji, na Kiokote, hawa hawakuwa maarufu?
Hao nao pia walikuwa moto sana na waliishi katika tabia zao kama watu kweli, baadae sana ndipo akazuka m'babe mmoja katika gazeti la Kiu anaeitwa Baba ubaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…