Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unakumbuka nini kuhusiana na gazeti la sani mwishoni mwa miaka ya themanini na mwazoni mwa miaka ya tisini?
Nimekumbuka enzi zile za gazeti la SANI, jamaa walikuwa wabunifu sana kwa matoleo yao,unamkumbuka kifimbo cheza na misemo mbalimbali(uchafuzi wa lugha?), kipepe na rungu lake, pimbi a.k.a dr. love yeye anatongoza kila demu! ndumila kuwili na wizi wake,aah wapi lodi lofa na kagari kake na kiko yake kitambi kule!madenge na vituko vyake akiwa na matanati yake !kuna mhusika moja hivi alikuwa chapombe sikumbuki alikuwa anaitwa nani vile?sukununu za babu sani je?wapi mechi ya bush star na born town?aah yale mazoezi kabla ya mechi hoiiii!uwanja wa fujo je? Hadithi za picha mambo ya kina Obi, Mzee Ole, Linda n.k ,wachapishaji walikuwa wabunifu kweli kweli, burudani zilizobebwa na wahusika wa kutengeneza lakini wanashambiiana na jamii!ilikuwa burudani sana kweli natamani ijirudie!
Wachoraji wa enzi zile ni kina John Kaduma(nasikia ni marehemu kweli?), Ibra Radi Washokera ndo ninaowakumbuka kama unakumbka wengine tukumbushane, watunzi wa hadithi pia walikua kina… aah km unakumbuka naomba tunikumbushe!
Jamaa walikuwa wakitoa toleo jipya basi wenye nazo wananunua then sisi wengine tunasubiria kuazima km ni shule basi utaona kikundi cha watu kibao wanasoma gazeti moja au km ni mtaani basi ndio kuazimana na ugomvi tele!natamani km nikusanye nakala za matoleo yale ya zamani!
Je wewe mdau unakumbuka nini katika gazeti la SANI?vipi kuhusu wahusika wake?hadithi na vituko je?
Kama unalikumbuka kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 80 basi pole.
Kipindi hicho lilikuwa limeisha kufa likichorewa na ma bongo fleva kama Ibra.
Mzee, Sani ni la miaka ya mwishoni ya Sabini hadi 1986. baada ya hapo ni makapi tu!
Mchoraji halisi wa Sani alikuwa marehemu Philip Ndunguru.
Huyu ndiye aliyewavumbua kina Lodi Lofa, Dr Love pimbi, Kipepe na Ndumilakuwili.
Ndunguru pia alikuwa anamchora Ndumilakuwili kwenye gazeti la Kenya Leo la Nairobi kule akimuita Kazibure na alikuwa maarufu hadi akatoa kitabu maalum cha Kazibure kilichouzwa kwa maelfu nchini kenya.
Philip Ndunguru pia ndiye aliyekuwa akisanifu majalada ya vitabu vya riwaya vya akina Musiba au Willy Gamba na watunzi wengine.
Mhariri orijino wa Sani ni marehemu Said S Bawji ambaye pia alitunga vitabu kama Usiku wa Balaa, Kisiwa cha Mayuku na A love story between Tanganyika and Zanzibar.
Sani pia lilikuwa na kibonzo cha mlevi Sokomoko kikichorwa na Ted Marealle!
Gazeti hilo pia lilikuwa ndio chimbuko la misemo ya mitaani kama vile, Utajaza, Kisebu sebu na Kiroho papo etc.
Upo hapo mkuu?
Kama unalikumbuka kipindi cha mwishoni mwa miaka ya 80 basi pole.
Kipindi hicho lilikuwa limeisha kufa likichorewa na ma bongo fleva kama Ibra.
Mzee, Sani ni la miaka ya mwishoni ya Sabini hadi 1986. baada ya hapo ni makapi tu!
Mchoraji halisi wa Sani alikuwa marehemu Philip Ndunguru.
Huyu ndiye aliyewavumbua kina Lodi Lofa, Dr Love pimbi, Kipepe na Ndumilakuwili.
Ndunguru pia alikuwa anamchora Ndumilakuwili kwenye gazeti la Kenya Leo la Nairobi kule akimuita Kazibure na alikuwa maarufu hadi akatoa kitabu maalum cha Kazibure kilichouzwa kwa maelfu nchini kenya.
Philip Ndunguru pia ndiye aliyekuwa akisanifu majalada ya vitabu vya riwaya vya akina Musiba au Willy Gamba na watunzi wengine.
Mhariri orijino wa Sani ni marehemu Said S Bawji ambaye pia alitunga vitabu kama Usiku wa Balaa, Kisiwa cha Mayuku na A love story between Tanganyika and Zanzibar.
Sani pia lilikuwa na kibonzo cha mlevi Sokomoko kikichorwa na Ted Marealle!
Gazeti hilo pia lilikuwa ndio chimbuko la misemo ya mitaani kama vile, Utajaza, Kisebu sebu na Kiroho papo etc.
Upo hapo mkuu?
Unakumbuka nini kuhusiana na gazeti la sani mwishoni mwa miaka ya themanini na mwazoni mwa miaka ya tisini?
Nimekumbuka enzi zile za gazeti la SANI, jamaa walikuwa wabunifu sana kwa matoleo yao,unamkumbuka kifimbo cheza na misemo mbalimbali(uchafuzi wa lugha?), kipepe na rungu lake, pimbi a.k.a dr. love yeye anatongoza kila demu! ndumila kuwili na wizi wake,aah wapi lodi lofa na kagari kake na kiko yake kitambi kule!madenge na vituko vyake akiwa na matanati yake !kuna mhusika moja hivi alikuwa chapombe sikumbuki alikuwa anaitwa nani vile?sukununu za babu sani je?wapi mechi ya bush star na born town?aah yale mazoezi kabla ya mechi hoiiii!uwanja wa fujo je? Hadithi za picha mambo ya kina Obi, Mzee Ole, Linda n.k ,wachapishaji walikuwa wabunifu kweli kweli, burudani zilizobebwa na wahusika wa kutengeneza lakini wanashambiiana na jamii!ilikuwa burudani sana kweli natamani ijirudie!
Wachoraji wa enzi zile ni kina John Kaduma(nasikia ni marehemu kweli?), Ibra Radi Washokera ndo ninaowakumbuka kama unakumbka wengine tukumbushane, watunzi wa hadithi pia walikua kina aah km unakumbuka naomba tunikumbushe!
Jamaa walikuwa wakitoa toleo jipya basi wenye nazo wananunua then sisi wengine tunasubiria kuazima km ni shule basi utaona kikundi cha watu kibao wanasoma gazeti moja au km ni mtaani basi ndio kuazimana na ugomvi tele!natamani km nikusanye nakala za matoleo yale ya zamani!
Je wewe mdau unakumbuka nini katika gazeti la SANI?vipi kuhusu wahusika wake?hadithi na vituko je?
Bila kusahau na lile gazeti la Mzee MEKO? alitoka kijijini kauza mazao yake akaenda town kununua trekta lakini akakutana na watoto wa mjini je mnakumbuka?
Sani lilikuwa jarida la ukweli! Wakati huo bado watanzania ni wajamaa kweli maana gazeti moja linasomwa na kijiji kizima(kwa sie tuliozaliwa vijiji).
Sikuwahi kuona gazeti jipya la sani, sababu yatu wote kusoma kopi moja ilikuwa inazeeka haraka. Nakumbuka kaka zangu waliokuwa wanasoma Dar wakija likizo lazima waje na sani. Fotokopi hazikuwepo watu wa stationary wangefaidi
Betina na nani yule bonge bonge...simkumbuki, walikuwa watu wa bifu kila wanapokutana..ila betina licha ya kuwa mwembamba alikuwa nammudu vizuri mwenzake bonge bonge