Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahihi kabisaUkiitwa PIMBI, NDUMILAKUWILI, LODILOFA ni tusi kubwa
Hahahaaa hili gazeti bado lipo nyumbani, mzee alikua mpenzi sana wa magazeti katengeneza mpaka library ya vitabu na magazetiHii ni Nakala ya gazeti la Sani la mwaka 1986 mwishoni kuelekea 1987 na kipindi hicho likiuzwa kwa shilingi 30 na Watanzania wakiburudika kwa katuni, hadithi, riwaya nk.
Wewe ulikuwa wapi kipindi hicho?
Tupe Taswira ya Taifa kipindi hicho (hata kama ulikuwa hujazaliwa ila umesoma au kuhadithiwa) katika nyanja za Elimu, Michezo, Burudani, Siasa nk.
Eleza kuhusu usafiri wa aina mbali mbali uliotumika miaka hiyo au hata kuweka picha zake.
Eleza kuhusu mavazi pendwa ya miaka hiyo na kila unachokijua kilitumia miaka hiyo na watu wa sasa hawavijui.
Lengo la uzi huu ni kukumbushana mambo ya miaka hiyo katika Taifa letu kwani wengine hawakupata fursa ya kuwepo miaka hiyo hivyo ni burudani tosha.
Picha ni muhimu sana....twende kazi.View attachment 1254454
Hahahaaa hili gazeti bado lipo nyumbani, mzee alikua mpenzi sana wa magazeti katengeneza mpaka library ya vitabu na magazeti
laizoni ilikuwa inabamba kinoma na nywele kubwa sikuhizi watu wanapenda kupiga viparaMuonekano wa vijana wa miaka hiyo. View attachment 1254653
Mambo namna hiiMiaka hiyo nilikua bado sijafika duniani,
lakini naona mavazi ya kwenye hiyo michoro ndio inavaliwa sasa hivi au fashoon imerudi?
Shikamoo kaka mkubwa,Nipe shikamoo yangu![emoji39][emoji39]
Mambo namna hii View attachment 1254656
Miaka hiyo niliamini Madenge ni mtu kweli anaishi Dar es salaam.Sikuwepo kipindi hiko Ila mshua wangu alikuepo na alikuwa mpenzi sana wa hayo majarida!
Alikuwa ananisumulia sana hasa alipokuwa akiniona nasoma vituko kwenye gazeti la Sani la siku hizi.
Tena BuguruniMiaka hiyo niliamini Madenge ni mtu kweli anaishi Dar es salaam.
Si unajua watu wafupi hawazeeki harakaHahahah kitambo sana ni vile tu hazeeki.
Basi siku zote nilijua unatokea kwetu Bunda.Nilikuwepo, japo nilikuwa dogo lakini nilijua kusoma na kuandika. Hili toleo lilikuwa linatoka mara 1 kwa mwezi mara mbili kama sikosei.
Nilikuwa moshi ambapo ndio kwetu. Nakumbuka kipindi hiko mabasi ya town trip kcmc, kiboriloni yalikuwa ni SHIMAWIMO. Yaani (SHIrika la MAendeleo WIlaya ya MOshi)
Kumbi za cinema zilikuwa mbili. ABC na Plaza Cinema. Nilikuwa sikosi kwenda pale plaza kila jumapili saa nne kuangalia sinema. Hata kama sijapewa hela na mshua lazima niende ongalao niambulie fungulia mbwa.
Masteling wa wakati huo, Amitha Batchan, Mithuny Chakraborty, Rish Kopoor,Rajesh Kumar, Denzolpa, kwa upande wa kina mama walikuwepo kina Jaya, Hemma Malini, nk.
Movie nazozikumbika, Nasseb,Amne Samne, nk. Kotambo sana.
Kumbi za disco zilikuwa ni Vijana club, Libert hotel iliyokuwa karibu na green view ambayo ilikuja kuungua baadae.
Mafuta ya kupaka wakati huo ni YOU na YOLANDA yaliyokuwa kwenye mkebe. Mengine ni rays, Ashanti. Wajanja walikuwa wanavaa jenzi na rabber mtoni kama Ascot. Suruali za kitambaa zilikuwa Cacha rell, Mr Dio nk.
Wahusika wa kuu kwenye kazeti la Sani. Kipepe, Lodi lofa, Sokomoka, Pimbi, Madenge,na Yule mpiga roba nani sijui nimemsahau.
Mc Sukununu.
Hadithi zilizowahi kutamba wakati huo kwenye gazeti la sani na mtunzi akiwa marehemu Hammie Rajab ni pamoja na Pumbazo La moyo, Usiku waGiza ya Joyce na Dalanda na kibibi Gula.
Dah muda umeenda aisee, ila kama juzi tu.
Kutili plaza? Kutili kabati ya mbeho? Enzi hizo ukitaka kuoa mchagga? Tv ilikuwa ni chuo cha polisi na chuo cha ushirika tu. Umesahau YMCA. Balozi wa Tanzania nchini Kuwait alikuwa form four chopra sec (mwanza sec school).Nilikuwepo, japo nilikuwa dogo lakini nilijua kusoma na kuandika. Hili toleo lilikuwa linatoka mara 1 kwa mwezi mara mbili kama sikosei.
Nilikuwa moshi ambapo ndio kwetu. Nakumbuka kipindi hiko mabasi ya town trip kcmc, kiboriloni yalikuwa ni SHIMAWIMO. Yaani (SHIrika la MAendeleo WIlaya ya MOshi)
Kumbi za cinema zilikuwa mbili. ABC na Plaza Cinema. Nilikuwa sikosi kwenda pale plaza kila jumapili saa nne kuangalia sinema. Hata kama sijapewa hela na mshua lazima niende ongalao niambulie fungulia mbwa.
Masteling wa wakati huo, Amitha Batchan, Mithuny Chakraborty, Rish Kopoor,Rajesh Kumar, Denzolpa, kwa upande wa kina mama walikuwepo kina Jaya, Hemma Malini, nk.
Movie nazozikumbika, Nasseb,Amne Samne, nk. Kotambo sana.
Kumbi za disco zilikuwa ni Vijana club, Libert hotel iliyokuwa karibu na green view ambayo ilikuja kuungua baadae.
Mafuta ya kupaka wakati huo ni YOU na YOLANDA yaliyokuwa kwenye mkebe. Mengine ni rays, Ashanti. Wajanja walikuwa wanavaa jenzi na rabber mtoni kama Ascot. Suruali za kitambaa zilikuwa Cacha rell, Mr Dio nk.
Wahusika wa kuu kwenye kazeti la Sani. Kipepe, Lodi lofa, Sokomoka, Pimbi, Madenge,na Yule mpiga roba nani sijui nimemsahau.
Mc Sukununu.
Hadithi zilizowahi kutamba wakati huo kwenye gazeti la sani na mtunzi akiwa marehemu Hammie Rajab ni pamoja na Pumbazo La moyo, Usiku waGiza ya Joyce na Dalanda na kibibi Gula.
Dah muda umeenda aisee, ila kama juzi tu.
Sababu ya avatar? Hapana mkuu, natokea kaskazini.Basi siku zote nilijua unatokea kwetu Bunda.