Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Wapo wakina Lodilofa,Pimbi,Njemba nchumali,Kiokote,Watoto mapacha,Komred kipepe mzee wa nyika,Mapung'o,Chepe,
Umenikumbusha kitambo sana mkuu.
 
Mie wa juzi juzi ila nilibahatika kusoma Sani na bongo. Kiasi ambacho nilikuwa nainjoi sana. Muonekano wa haya majarida ulichangia. Wale wadada duuuh sijui tu na vile vijinguo. Aiseeee nilikuwa napenda sana kuyasoma
 
Kijarida cha wahenga enzi hizoView attachment 1259900
Wengi hawajui kuwa, gazeti hilo lilianzishwa na watu wawili. SAID BAWJI, na NICO YE MBAJO. Majina ya mwanzo ndiyo yalitengeneza jina SANI. Lakini baadaye Nico alijitoa, na kuanzisha gazeti lake (jina limenitoka kidogo).
Alipokuja kufariki SAID BAWJI, kaka yake aitwaye AMRI BAWJI, aliliendeleza kwa muda, na wakati huo huo, akaanzisha gazeti jingine liitwalo AMBA.
Historia inabaki kuwa, gazeti la SANI ndilo baba wa majarida yooooote ya namna hiyo!
 
Hivi Baba la Baba Sesten Zakazaka na wewe ulisomaga hivi vijarida au ndio kama mie tu. 😅😅😅
Sshadeeya nadhani toleo la kwanza la Sani ninalo, yaani marehemu Mzee alikua akinunua wakati huo na mimi nikiyahifadhi yote!

Ninayo nimeyahifadhi mengi mpaka pale alipofariki Said Bawji ambaye ndie mwanzilishi wa gazeti hilo ndio nikaacha maana hata muelekeo wa story na maudhui vikabadilika
 
Wengi hawajui kuwa, gazeti hilo lilianzishwa na watu wawili. SAID BAWJI, na NICO YE MBAJO. Majina ya mwanzo ndiyo yalitengeneza jina SANI. Lakini baadaye Nico alijitoa, na kuanzisha gazeti lake (jina limenitoka kidogo).
Alipokuja kufariki SAID BAWJI, kaka yake aitwaye AMRI BAWJI, aliliendeleza kwa muda, na wakati huo huo, akaanzisha gazeti jingine liitwalo AMBA.
Historia inabaki kuwa, gazeti la SANI ndilo baba wa majarida yooooote ya namna hiyo!
Mkuu Nico Ye Mbanjo alianzisha jarida la MCHESHI lililokua na michoro ya kina dada wenye maumbo yaliyokazia sana
 
Mkuu, shukran kwa kunikumbusha. Na huyo Nico, ndiye aliyekuwa anachora, ile miaka ya mwanzoni lilipoanzishwa hilo Sani. Lakini kiboko ya uchoraji akaja kuwa Philipo Ndunguru.
 
Ni kweli Mkuu, Philip Ndunguru ndio mchoraji wa katuni orijino za kina Kipepe, Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Mwinyi Mpeku na hata kumchora Mzee Sani mwenyewe
 
Sshadeeya nadhani toleo la kwanza la Sani ninalo, yaani marehemu Mzee alikua akinunua wakati huo na mimi nikiyahifadhi yote!

Ninayo nimeyahifadhi mengi mpaka pale alipofariki Said Bawji ambaye ndie mwanzilishi wa gazeti hilo ndio nikaacha maana hata muelekeo wa story na maudhui vikabadilika
Saafi sana Muhenga. 🥰

Mi nayasikia tu love hata sikumbuki kama nshawahi kuyaona. 🙈🙈
 
Aisee......
Chepe, mjomba Kobelo, Meko, Komred kipepe, Madenge na kadhalika. Hawa ndio walikuwa wasaka kabumbu wa team ya Bush Stars.
Ebu weka kumbukumbu sawa mkuu

Meet Mr. Chepe from Bongo
 
Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    37.1 KB · Views: 7
Back
Top Bottom