Unakumbuka nini kuhusu mgomo wa madaktari mwaka 2012?

Unakumbuka nini kuhusu mgomo wa madaktari mwaka 2012?

Joined
Jul 15, 2026
Posts
64
Reaction score
187
Bila kupoteza muda, nadhani wengi tunakumbuka kuwa mwaka 2012 kulikua na vuta ni kuvute za hapa na pale baina ya Madaktari nchini na Serikali chini ya aliyekuwa Rais wa kipindi hicho Dr. Jakaya Marisho Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (mzee wa “utapigwa tu”), issue ambayo ilipelekea chama cha madakatri kuitisha mgomo wa nchi nzima na kupelekea serikali kuagiza madaktari wa jeshi kuingia mahosipitalini kwaajili ya kutibu raia.

Binafsi nakumbuka sana tukio la Ulimboka kutekwa na kupigwa vibaya mnooo.

Anyway, tutakumbuka pia mgomo huu hatari zaidi kuwahi kutokea katika nchi yetu ulisababisha aliyekua Mwanasheria mkuu wa serikali wa kipindi hicho kupeleka maombi ya zuio la mgomo huo mahakamani ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania, Division ya kazi, Dar es Salaam chini ya Jaji Moshi ilitoa amri ya zuio ya mgomo huo kwasababu kubwa kwamba, kama mgomo huo ungeruhusiwa na amri hiyo isinge tolewa basi madhara makubwa ambayo yasingeweza kufidika yangetokea ikiwemo vifo.

Madakatri wao walikua wakidai kwamba hata walipokuwa wakitoa huduma watu walikua wakifariki kutokana na kukosa huduma stahiki na mazingira mabovu ya kazi kwaio walisema mgomo huo ulikuwa pia ukilenga kuilazimisha serikali kuchukua hatua za haraka ili kuboresha huduma za afya nchini.

Kwa upande mwingine madaktari walihitaji waongezewe posho ya kuitwa kazini kutoka 10k mpaka 25k, pia walitaka kuongezwa posho ya uchunguzi wa maiti kutoka 10k mpaka 100k na jingine ni kuwa walitaka uongozi wa juu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ubadilishwa mara moja.

Kutokana na mgomo huu, Dr. Haji Mponda aliyekua Waziri wa Afya aliondolewa madalakani yeye pamoja na aliyekua katibu mkuu wa wizara hiyo Dr Brandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali Dr Deo Mtasiwa na kisha Dr Hussein Ally Mwinyi akawa ndiye waziri wa wizara hiyo.

Licha ya mabadiliko hayo ya uongozi madaktari walidai baadhi ya ya madai yao ya msingi bado hayajafanyiwa kazi na hivyo kupelekea kutangaza mgomo mpya mnamo tarehe 21 June 2012 .

Pia tunakumbuka vyema kuwa mgomo huu ulikua ukiongozwa na Dr. Steven Ulimboka ambaye alikua ndiye mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) ambapo alilipotiwa kutekwa na watu wasiojulikana siku 5 tu kutoka kutangaza mgomo huo yani tarehe 26 June 2012 maeneo ya leaders club Dar es Salaam.

Ulimboka alitekwa wakati alipokuwa katika mazungumzo juu ya mgomo huo na mtu mmoja aliyemuita na kujitambulisha kama Abed na Afisa wa serikali kutoka ikulu na kuja kuonekana kesho yake katika msitu wa Mwabepande uliopo bunju Dar Es Salaam na ndipo msamalia mmoja alimuokota na kumpeleka kituo cha polisi Mwabepande ambapo hapo Dr ulimboka alifatwa na aliyekua Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu wa wakati huo Bi. Helen Kija ambaye nae alisema kuwa licha ya jitihada zake za kupigia ambulance kutoka muhimbili kugonga mwamba na kuamua kumkimbiza Dr Ulimboka hospitalini kwa kutumia gari yake binafsi laki bado njiani hapo walikutana na vikwazo mbalimbali ikiwemo foleni na uwepo wa gari moja iliyokua ikiwazinga mbele yao ili kuwachelewesha hospitali japo baadae walipatiwa msaada wa ambulance kutoka katika shirika la afya la AAR ambapo lilimpeleka Dr Ulimboka mpaka moi ambapo alilazwa kwa muda kabla ya kwenda nchini South Africa kwa matibabu.

Hii issue ya Ulimboka iliacha mjadala mkali sana ikiwa swali kuu ni je, ni kina nani waliomteka Ulimboka??.

Gazeti la mwanahalisi liliwahi kuchapisha habari iliyosema “Aliyemteka Ulimboka huyu hapa” ‘Ni Ighondu wa usalama wa Taifa’ habari ilisema kwamba aliyemteka Dr Ulimboka ni Ramadhani Ighondu na kuwa ndiye afisa wa usalama wa Taifa aliyekua katika mzungumzo na Dr Ulimboka, dakika chache kabla ya kutekwa kwake, jambo ambalo lilisababisha serikali kulifungia gazeti hilo kwa muda usiojulikana kwa kosa la kuandika habari za upotoshaji na uchochezi.

Jakaya Kikwete yeye alitangaza kuwa serikali yake aihusiki kivyovyote na utekaji huo wa Ulimboka na wakati huohuo Waziri mkuu Pinda naye akiliambia bunge kuwa serikali aihusiki na utekaji wa Ulimboka.

Siku chache baadae kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi, Dar Es Salaam wa wakati huo Suleiman Kova alidai kuwa wamemkamata mtu mmoja aitwae Joshua Malundi (21) kutoka kenya ambaye amekiri kuhusika na kumteka na kumtesa Dr ulimboka, Kova alisema kuwa mtu huyo alienda kutubu makosa yake katika kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo kawe Dar Es Salaam hata hivyo Ngwajima ambaye ndiye kiongozi wa kanisa hilo, alikanusha kauli hiyo ambapo hata Joshua naye baadae alikanusha kauli hiyo na kisha kupewa adhabu ya kifungu cha mwezi mmoja jela pamoja na fine ya 1000 aliyolipiwa na moja ya waandish wa habari kwa kosa la kulipotosha jeshi la polisi.

Pamoja na hayo yote mpaka leo hakuna mtu yeyote aliyethibitika kama mtejaji wa Dr Ulimboka na kitu kinacho nishangaza mimi mpaka leo hii na wadau wengi waliokuwa wakifuatilia suala hili ni ukimya aliokuwa nao Dr Ulimboka kulizungumzia suala hili

Najiuliza Why aliamua kulikalia kimya kabisa suala hili licha ya kufatwa na mamia ya waandishi wa habari kutaka kumuhoji juu ya suala hili toka alipotoka nchini SA kwa matibabu, au kuna nguvu ilitumika kumkalisha kimya..???
 
Yule Dokta Ulimboka walivyomnyofoa meno

Alikuwa Daktari kutoka Private akaenda kwenye mgomo wa madaktari wa serikali
 
Kwasasa huyu mwamba anaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambako amekuwa akiendesha maisha yake ya kawaida na ya faragha tangu alipopona majeraha makubwa aliyoyapata.

Baada ya kufanyiwa ukatili huo wa kutisha mnamo Juni 2012—ambapo alitekwa, akapigwa vibaya, na kung'olewa kucha na meno katika Msitu wa Pande wakati akiongoza mgomo wa madaktari—alipelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya dharura yaliyookoa maisha yake.

Aliporejea nchini, alizuiliwa kufanya kazi ya utatibu katika hospitali za umma, hali iliyomfanya ageukie shughuli binafsi za kiuchumi huku akichukua tahadhari kubwa za kiusalama na kuepuka kuonekana hadharani. Katika matamko yake machache kwa vyombo vya habari, Dk. Ulimboka alifafanua kuwa ukimya wake haukutokana na kuhongwa wala kutishwa, bali ulikuwa ni uamuzi wa kulinda afya yake na kufuata ushauri wa madaktari, ingawa mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa au kuwajibishwa kisheria kwa unyama huo aliofanyiwa.
 
Hamis Kigwangala alichomokaje na hii ishu. Nakumbuka na yeye alikua ni mmoja wa viongozi wa madokta
Kigwangala mwanasiasa yule hana lolote alikuwa anajifanya kukaza halafu baadae anajifanya kuiambia serikali itafute muafaka na madaktari wakati madokta walihimiza mgomo wakijua wakienda meza ya mazungumzo yatakuwa yale yale danadana za kisiasa.
 
Ule utekaji ulikuwa km movie hivi , maana baada ya kumteka gari ilizunguka ile Bar kwa mida kustopisha gari zingine kwa dakika kadhaa

Lile tukio nililifatilia sana humu ndani teena liliandikwa kiufasaha haswa.
 
Bora yale meno walifanya kuyavunja maumivu yake ni ya muda tu ila kunyofolewa kucha na pliers aisee maumivu yake utayasikia milele.

Jamaa baada ya lile tukio alikaa kimya kama mbwa koko aliyepoteza windo yaani kimyaa!
Daaah ule ulikuwa ni unyama uliokithiri.

Kwakweli kwa ukatili ule asingeweza kubaki na ujasiri ule wa mwanzo.
 
Back
Top Bottom