Unakumbuka nini kuhusu mgomo wa madaktari mwaka 2012?

Licha ya kua umeiba habari toka kanyamala media huko Facebook, lakini umenikumbusha mbali sana ilikua 2012 ,moja ya skendo kadhaa za utekaji zilizoihusu serika ya JAKAYA KIKWETE
 
Huu mgomo ulikuwa Game Changer kwa madaktari wote nchini

Halafu HUWEZI amini, madaktari wote nchini hadi wanafunzi wa udaktari walimchangia matibabu ya Dr. Ulimboka na kusafirishwa kwenda Afrika Kusini
 
Hakupaswa kukaa kimya, mbona Tundu Lissu yupo ngangari ijapokuwa nae alichungulia kifo?
 
Dah nipo f1 apo ila huu mkasa naukumbuka
 
Bora yale meno walifanya kuyavunja maumivu yake ni ya muda tu ila kunyofolewa kucha na pliers aisee maumivu yake utayasikia milele.

Jamaa baada ya lile tukio alikaa kimya kama mbwa koko aliyepoteza windo yaani kimyaa!
Mkuu meno ni kitu kingine..
Mtu awezi kufa kwa kutolewa kucha... Ila meno weeeh
 
Dr Ulimboka alikwenda kuishi Marekani kwa kumbukumbu zangu,sijui kama baadae alirudi Bongo. Nakumbuka siku anarudi kutoka Sauzi kwenye matibabu alivyopokelewa Airport kwa shangwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…