LOL pole sana,hakuna urafiki kati ya nyoka na mwanadamu,hasa blackmamba,waliomuua walifanya sahihi,pole leo hii tusingekua tunapata nondo zako walahiAsubuhi saa 12 naamka na wenge nikimbie shule.. naenda kushika kitasa ili nifungue nakuta black mamba kajizinga pale kwenye kitasa ananikodolea macho..
Yaani umbali wa nyoka na mkono wangu kama inch 5 tu.
Nilishtuka sana..hua siui mdudu yoyote baada ya mbu so niliamsha wengine waje wamtoe nikawaambia wamfukuze nje. Bahati mbaya wale binaadamu walimuua yule nyoka
Pole sana ndugu.Mmmh.. .
Nilikaa I.c.u..mda sana tu..
Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!
Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!
Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante .. ...Pole sana ndugu.
Kweli kabisa Mkuu.Kusali ndio mambo yote.Mungu ni Mwema.Asante .. ...
Tusali sana kila mtu kwa imani yake..
kuna vingi vya ajabu..ambavyo vipo ila hatuvioni!
Unapoamka mpa kuja kulala tena ukiwa mzima...mshukuru Mungu sana!
Sent using Jamii Forums mobile app
Lol pole Sana Mkuu,Mwache Mungu aitwe Mungu.Mwaka 98 maeneo ya mazizini unguja kituo cha polisi ilikua kuna gari 2.8 inatoka airpot imekolea kama spidi 80 mimi nina vespa nilimpakia kaka yangu niliingia katikati ya gari ikatupiga mzinga mkubwa sana ikatuburuza kama mita20 sikujua dereva alisimama kwa kutumia nini.ulikua ni uokovu wa Mungu tu kutoka wazima tulichunika na mimi nikapasua sped meter kwa kichwa.
Nikiwa na miaka 13 nilianguka kwenye mti mrefu kuanzia juu mpaka chini nikagongana na matawi mpaka nikafika chini kabisa. Nilijifuta mavumbi tu.
Black mamba ni mpole sana tena sana, ila uisilmbe aliamshe!!!.lee van cliff, Huyo hakuwa Koboko.... (Black Mamba). Manake huyu hana simile .. haujamchokoza lakini anakutoa nduki.
Mimi siamini kwenye "God intervention" kila jambo linafuata misingi na kanuni za asili... hapo ilikuwa nyoka akugonge au akuache, au wewe umuue. Hakuna cha ajabu hapo (hakuna kanuni iliyovunjwa).
Nyoka kuingia ndani kwako inawezekana, nyoka kukudhuru au kutokukudhuru inawezekana pia.
Jiulize hivi angekugonga je, ungesema nini kuhusu Mungu (virse versa ??)
Sent using Jamii Forums mobile app
Lol pole Sana Mkuu,Mwache Mungu aitwe Mungu.
Baada ya kunusurika huyo mwenzako ulimzaba au hukumzaba makofi? AhsanteNilikuwa naendesha gari,ghafla nikaona mdudu anatembea kwenye kidole changu,nikawa nafungua dirisha ili nimrushe kwa nje,ile niko katika harakati za kunyanyua mkono nimrushe,mwenzangu akaniambia kuna gari tunaligonga,lilikuwa linakuja opposite direction,wakati naangalia mbele ni kweli nimehama njia ila liko mbali kidogo na ile gari,na dereva wa lile gari alikuwa tayari ameshasogea pembeni kwani alishaona nimeyumba,niko katika harakati za kurudisha gari upande wangu yule mwenzangu akawa amenivuta mkono nilioshika sterling,kwakweli kilichotokea pale ni kwa neema ya Mungu tu tuko hai mpaka leo,gari iliyumba kama mara tatu huku tairi za upande mmoja zikiwa tayari juu,nikatumia ufundi wangu wote mpaka gari ikatulia,thanks God am still alive...
Yani hiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,kwa sauti ya mkulu pombe[emoji16][emoji16]Sikuamini kabisa kama ingetokea katika maisha yangu ,yani bila kutazamia ilitokea tu! Kwa kweli kuna mambo yanaweza kutokea bila kuzaniwa wala kufikiri ila nazani ni kwa ajiri ya maombi ya wengi hali yoyote inaweza kujiri.
Kwa kweli siamini hadi leo kama naweza kuwa hapa,yani ilikuwa mwaka 2015 miezi ya mwishoni ambapo mimi nilikuwa katika shughuri zangu mida ya saa 7 mchana maeneo fulani,alipita jamaa mmoja ambaye sikuzani kama angeweza ila ndo ikaja kuwa ,ndo huyu tunaye sasa ni JOHN POMBE MAGUFURI akiomba kura kwa wana nchi wa Tanzania na baada ya hapo akashika hatamu ya kuongoza nchi, dah siamini kabisa,jamaa anapiga kazi sijawahi ona,yani hata huyo nyoka wako angemuona huyo jamaa angetoka speed ya jet.viva POMBE
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu,nilimsamehe kwakuwa inawezekana hakuwa yeye,kwani mpaka sasa siamini kama ni kwa akili zake angeweza kufanya tukio la hatari kama lile na hata yeye alijilaumu sana kwanini alichukua ule uamuzi...Baada ya kunusurika huyo mwenzako ulimzaba au hukumzaba makofi? Ahsante