Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Mmmh.. .

Nilikaa I.c.u..mda sana tu..

Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!

Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!

Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!



Sent using Jamii Forums mobile app
watu wa Astra projection wanajua hii kitu. Nawaza ingekuwaje ndugu wangedhani umekufa wakataka kukuzika...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa dalasa la sita siku hiyo niliamua kujisomea usiku, so nilikuwa nasoma kwa kutumia kibatari, nilikuwa nasoma huku nimelala kitandani na kibatari kiko pembeni kidogo juu ya meza, nilipitiwa na usingizi kumbe mto wa sufi niliokuwa nimejiegemeza uliangukia kibatari ukaanza kuwaka na nilikuwa nimelala na babu yangu ambaye alikuwa haoni vzr na kutembea kwa tabu sababu ya uzee pia kilichosaidia huyu babu yangu tulilala vitanda tofauti!

Aise mto wote uliungua babu akaita sana sikusikia sababu ya usingizi mzito makelele ya babu ndio yaliyowaamusha watu wakaja kuvunja mlango godoro la Sufi limeanza kushika moto na chumba kimejaa moshi, aise sielewi ule usingizi ulitoka wapi maana pamoja na makelele ya babu sikusikia, watu waliita sana kwa nje sikusikia hata walivyovunja mlango sikushtuka wakanibeba kunitupa nje ndio nashtuka,
Mpk Leo naamini ni Mungu alitusaidia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh aisee hawakukushambulia kwa matusi au makofi labda, maana hapo lazima raia walionyesha hasira kali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mungu yupo man
Siku moja tulikua site
Tunafanya maintenance kubadiri nguzo ya HT...kuangalia belt(kwa wasioijua Ni ule mkanda wakujifunga kiunoni unakushikiza na nguzo unavyokua juu) kuchek belt yangu imefunguka Ile lock yake
Dah afu nipo kama meter 12 juu

kelphin kepph
Tena ndio uwe kama umelala yombo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yako mambo mengi sana ni kweli Mungu kayafanya hasa nizungumzie ajali.
1. Ilikua 2015 nko kwenye roli Benz Actros 15 tonnes hi gari inakimbia jamani, bahati mbaya akatokea mwanamke anakatisha barabara bila tahadhari tukamkwepa na kuingia site nyingine kuna pikipiki tukamkwepa tena na mbele kuna kona kali na kituo cha daladala ikabidi tubetue gari ikalala barabarani tuliburuzika sana ila hakuna mauti iliotokea pale lakini baada ya masaa mawili lilianguka roli jingine pale pale na kuua watu nane.
2. X-mass ya 2019 juzi hapa nimetoka shamba nawahi ibada barabara ni rough road gari ilipoteza mwelekeo nikavamia kichuguu gari ikarushwa hewani kurudi barabarani tairi zikiwa juu ikajigeuza na kutua chini tairi zikiwa chini, No ni Mungu aligeuza na tukatua salama atukuzwe yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa naendesha gari,ghafla nikaona mdudu anatembea kwenye kidole changu,nikawa nafungua dirisha ili nimrushe kwa nje,ile niko katika harakati za kunyanyua mkono nimrushe,mwenzangu akaniambia kuna gari tunaligonga,lilikuwa linakuja opposite direction,wakati naangalia mbele ni kweli nimehama njia ila liko mbali kidogo na ile gari,na dereva wa lile gari alikuwa tayari ameshasogea pembeni kwani alishaona nimeyumba,niko katika harakati za kurudisha gari upande wangu yule mwenzangu akawa amenivuta mkono nilioshika sterling,kwakweli kilichotokea pale ni kwa neema ya Mungu tu tuko hai mpaka leo,gari iliyumba kama mara tatu huku tairi za upande mmoja zikiwa tayari juu,nikatumia ufundi wangu wote mpaka gari ikatulia,thanks God am still alive...
 
Nikiwa nimejilaza kitandani kwa kupumzika tu,miguu iko chini, yaani nilikaa kitandani halafu nikaamua kujilaza. Nilikaa kwa upande ambao mtu akiwa amelala kawaida huweka au kuelekeza miguu yake, baadae nikajilaza.

Baada ya dakika kadhaa nilimuona nyoka akinitazama, akiwa amesimama upande wa kushoto wa kitanda, tukawa tunatazamana yeye akiwa chini sakafuni. Tulitazamana hatimae nyoka akaamua kushusha kichwa chake na kugeuka na kuondoka zake.

Niliishiwa nguvu, sikuamini kabisa nilichokiona.yaani kitendo cha kuinuka nusu mzima nyoka ndio kilinishangaza, hapo ndipo nilipojua kuwa kumbe nyoka anaweza kupanda kitandani kirahisi tu.

Naamini ni Mungu tu ndio alikuwa mwamuzi wangu siku hiyo.

Unaamini katika Mungu? Wewe ulinusurika vipi, uliokoka vipi? Ulipona vipi? Tuwekee tukio lako tafadhali.

Huwezi ukahesabu matukio makubwa na ya ajabu anayokuepusha nayo Mungu kimiujiza hata ndani ya dakika moja tu, ni mengi muno kiasi kwamba akili yako haina uwezo huo. Kwa hiyo hili swali lako katika uhalisia haliko sahihi!
Tuchukulie mfano, ukitoka nyumbani asubuhi halafu ukarudi jioni, ni muujiza wa ajabu mno ambao watu wengi huwa hatuelewi ila ni kwa sababu tu kuwa tulio wengi huwa tunatoka salama na kurudi salama, na kwa sababu hiyo tulishachukulia kuwa ni granted na ni kawaida, na si muujiza. Kwa hiyo katika hili huwa wengi wetu tunashindwa kuuona mkono wa ajabu wa Mungu katika haya yote ya kila siku, unless mtu anusurike kwenye tukio kama la kukoswa koswa na moto wa tank la mafuta, hapo ndiyo tunadai kuuona muujiza wakati kumbe Mungu huwa hata katika hali tofauti na hiyo, huwa anatuepusha na matukio mengine mengi makubwa sana, na wakati mwingine ya ajabu kuzidi hata yale ambayo huwa anatuonyesha, lakini huwa hatuuoni muujiza wake kwa sababu tukio hakutuonyesha; aliamua kulimeza mwenyewe na sisi tukawa hatukuliona. Na pale anapoamua kutushirikisha katika kuliona tukio, ndiyo pale tunapoona kuwa ametenda muujiza wakati katika hali ya kawaida, every coming second Mungu yuko na wewe na anatenda miujiza ya ajabu sana kwako, bila wewe mwenyewe kujua. Mungu akiamua kukuacha wewe just a second, YOU ARE GONE! Kwa hiyo ninachoweza kusema ni kuwa Mungu anatenda muujiza kwako kwa idadi ambayo matukio yake huna uwezo wa kuyahesabu kwa namna yalivyo mengi, tuseme hata ndani ya dakika moja tu,! Anatenda kimya kimya bila kukuonyesha.
Nilishangaa sana siku moja tuko kwenye mkutano wa nje wa injili, mhubiri mmoja akajisifu kuwa ana uwezo wa kujilinda dakika 15 bila Mungu. Hii possibly ilikuw ni shibe ya chakula kwa sababu ilikuwa jioni. Alikuwa ameshiba!
 
Nilikuwa naendesha gari,ghafla nikaona mdudu anatembea kwenye kidole changu,nikawa nafungua dirisha ili nimrushe kwa nje,ile niko katika harakati za kunyanyua mkono nimrushe,mwenzangu akaniambia kuna gari tunaligonga,lilikuwa linakuja opposite direction,wakati naangalia mbele ni kweli nimehama njia ila liko mbali kidogo na ile gari,na dereva wa lile gari alikuwa tayari ameshasogea pembeni kwani alishaona nimeyumba,niko katika harakati za kurudisha gari upande wangu yule mwenzangu akawa amenivuta mkono nilioshika sterling,kwakweli kilichotokea pale ni kwa neema ya Mungu tu tuko hai mpaka leo,gari iliyumba kama mara tatu huku tairi za upande mmoja zikiwa tayari juu,nikatumia ufundi wangu wote mpaka gari ikatulia,thanks God am still alive...

Ni Mungu sio ufundi wako. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji120]
 
Mwezi wa 10 mwaka jana nipo home alone, nina stress kali, nimenunua chupa ya konyagi na sigara. Namaliza konyagi nawasha sigara. Navuta nikiwa nimejilaza kitandan. Napitiwa na usingizi. Naamka usiku sana nakuta shuka na neti vimeungua sehem kubwa kidogo. Najiuliza mpaka leo, ni nani alizima ule moto? Hakika nilistaajabu uwepo wa Mungu. Kwa kweli [emoji120][emoji24][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
aisee,ila cha ajabu hadi hapo sijaona sehem uliyosema umeacha pombe,hahahhaaaaa
 
Saving hope... Utakua uliangalia hii muvi
Mmmh.. .

Nilikaa I.c.u..mda sana tu..

Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!

Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!

Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom