Nikiwa na miaka 8 au 9...nilimkwepa mshua nkazuga naenda kuteka maji na sufuria...ilibidi niende kweli,kufika pale nilimkuta Dada anafua pembeni ya kisima...nikamsalimia nkaingia na sufuria yangu pembeni ya kisima...sijui mawazo au Nini,loh sufuria ikaponyoka ...katika kupambana isizizame,nkatelezea na Mimi ...nshaanza kunywa vikombe kadhaa...bahati yule Dada anafua alikua amemaliza maji anakuja kuteka mengine...loh ndo kaniokoa
1 Form 3 I think...nilikua napenda Sana michezo zaidi basketball,Kuna siku tulitoka kwenye mazoezi ya viungo magumu kidogo
Sasa shule yetu mipira ilikua imeharibika na tulikaa bila mipira kwa siku nyingi....kwahiyo kipindi Cha michezo muda mwingi tuliutumia kwa mazoezi ya viungo na riadha
Siku tunatoka mazoezi Mara tukapewa mipira mipya na mkuu wa shule,kwa ajili ya munkari siku niliopt kucheza football
Rafiki angu Ray alishauri nisicheze kwa sababu tulikua tumefanya zoezi Kali kidogo
Nilipangwa no Saba pembeni
Nakumbuka ilipigwa pasi ndefu Sana kwangu,nkawa naiwahi isitoke nje kwa Kasi,nikataka kuutudisha ndani mpira kwa kisigino
Lahaula[emoji21][emoji21][emoji21]kwa spidi yangu na mpira,nilijikuta nimeupanda ule mpira kwa juu nikasafiri nao mita kadhaa,kabla ya kurushwa juu na kuangukia kichwa kwa kisogo
Nakumbuka niliinuka,lakini ghafla nkaona narudi chini,na kuhisi nagandamizwa na uzito mkubwa kutosimama Tena,niliona naanza kupata taabu kupumua...nkasikia kwa mbali watu wanapiga mayowe anakufaa
Kilichoendelea siku jua,nilishtuka nesi ananichoma sindano....nkamuuliza kwani vipi,mbona unanichoma...kumbe nilivyoanguka,nikianza kutoa povu na damu,na wengi walikimbia...wachache jasiri walikuja kunipepea mpaka nkawa kwenye Hali ya kawaida kiasi
Naambiwa nilikua naongea Mambo yasioeleweka,mpaka leo tukio hili nahisi limeniathiri kiasi....Nina tatizo kubwa la kusahau
Mwaka huu chimbo Fulani,niliumwa tumbo na mgongo kwa nusu saa,kiasi nikianza kusufforcate kupumua,nkajua navuta,nililia Kama mtoto huku nasali,mbaya ilikua mbali na hospital... ntashukuru nilitoka mzima
Ya wanaosema kufanyiwa ushirikina Ni mengi,ila Sasa sina uhakika,Kama kweli au lah
Hizo Ni hatari nilizoziona,lakini naamini ziko nyingi Mungu kanikinga na anaendelea kunikinga ambazo sizifahamu pia
Sent using
Jamii Forums mobile app