Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Matukio yayanafanana,nakumbuka nikiwa miaka fulani hivi kwenye nyumba ya Asili nimelala kifua wazi Nyoka akaniangukia kifuani nikamrusha na mkono "automatically " jasho lilinitoka nakahisi kufa nyoka akashika njia yake nami nikakimbia nje nahema natazama kama kaningata kifuani. Hakika Mungu anasaidia!
Aiseee Mungu ni mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lee van cliff,
MUNGU yupo jaman kwa yaliyonitokea hakika alisimama mwenyewe
mtu anakupa tuhuma za uongo na zaidi ni za jinai kubwa ila anasuka maneno na ushahidi wa uwongo hatari sana.. sitakaa nimuamini tena kiumbe kinachoitwa mwanaadam .

yaani yalivyonikuta ndio nilielewa kwanini misholi eliud aliimba 'simama mwenyewe bwana'
 
MUNGU yupo jaman kwa yaliyonitokea hakika alisimama mwenyewe
mtu anakupa tuhuma za uongo na zaidi ni za jinai kubwa ila anasuka maneno na ushahidi wa uwongo hatari sana.. sitakaa nimuamini tena kiumbe kinachoitwa mwanaadam .

yaani yalivyonikuta ndio nilielewa kwanini misholi eliud aliimba 'simama mwenyewe bwana'
alikuwa mwanamke??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukubwani
Tukiwa grocery Mbagala..tunakunywa na wenzanhu ukazuka ugomvi wa uonho na kweli kisha ukatulia.
Mimi nikasimama krb na ukuta sina hili wa lile..
Mwanzishili wa ugomvi akasimama mkabala na mm umbali wa hatua tatu tu,ameshika chupa ya bia.
Akasema wewe unajfnya unajua...kufumba na kufumbua kbl sjajibu kitu chochote..
Nikaskia mbengerembengere ukutani na sakafuni..
Hee kumbe chupa ilikosa shabaha usoni mwangu..
Ilikuwa jmosi..kesho yake asbh jpili nilienda church kutoa sadaka ya shkran nikiwa na pombe kichwani,nimekoswa na chupa usoni.

Udogoni
Nikiwa nimesimama pmbn ya kisima mm na rfk zangu watatu..
Nilistukia nyuma nimesukumwa, punde kufumba na kufumbua nikajikuta natapatapa napiga mbizi ili kujinusuru nisinywe maji..
Haikupita hata dakk mbili nikajikuta navutwa mkono na mmoja ya wale tuliokuwa nao..
Jicho jekunduu,tumbo top top..nguo zimelowa balaa nilikuta hata siwezi kupigana na aliyenisukuma ni dogo tu nilikuwa nina mmudu..
Home ht sikusema nilikaa kimya licha ya kuulizwa kwann nimelowana,niliishia kudanganya.
Hadi leo hawajui niliwahi kusukumwa kusimani.

Udogoni
Ivi unavikumbuka vile vyoo vya tundu la kulenga shabaha za kimba.
Eheeeee hivyohivyo..
Kule kwetu walijengaga mtundu mkubwa kiasi ambacho ukichuchumaa unajihisi uko labor..
Sasa nikabanwa nikaenda kupunguza vitu flan vya tumboni..
Nika jitegesha mguu pande nika fit nika push makimba ya kutosha nikanyanyuka..kbl sijatoka nikaanza mchezo wa kusukuma majivu kwa mguu mmoja ili mende wazame chini zaidi..
Heeeee mweee mguu ukateleza kuingia tunduni' nikajikuta mikwapa yamenasia huku na huku juu ya vitofali...huku
Tumbo,kiuno na miguu ikiwa inapunga joto la kinyesi huko chini...
Kwa sabb ya wembamba wangu
..nikaanza kujivuta juu...nikajivuta zaiidi mpk nikatoka..
Aiserr nilitoka na uchafu uchafu wa pmbzn mwa tundu la choo na majivu n.k nikajikausha sikumwambia mtu.

Nikikumbuka haya na Menghine kwa uvivu tu wakuandika,Nasema ni mkono wa Bwana.
 
Siku moja kama saa 2 usiku natoka zangu magomeni mataa naelekea fire natembea kwa mguu upande wa kulia wa barabara ya magari yanayoelekea magomeni mataa.Kwa mbali nawaona watu kadhaa mbele wanasafari zao lakini wanakuja nakotokea mimi japo bado hatujapishana.Na wao walikuwa upande niliokuwa natembea mimi

Baada ya kutembea hatua kadhaa nahama upande wa kulia wa barabara nahamia katikati ya barabara mbili mle zilipokuwa taa zile ndefu za barabarani ambapo sasa vimewekwa vituo vya mwendokasi.

Lengo langu la kuhamia katikati ya barabara mbili lilikuwa ni kujiandaa nivuke nitembee upande wa kushoto wa barabara ya magari yanayo elekea Fire.Cha ajabu nilipotoka kulia mwa barabara nilipoingia katikati ,kuna watu watano nao walihama wakawa wanatembea katikati ya barabara mbili kama mimi ,nilipotoka katikati na kuvuka kwenda kushoto katika wale watu Watano watatu nao walihamia kushoto kama mimi na wawili wakabaki katikati.Wale waliohamia kushoto wakawa wanatembea sasa tunaelekea kukutana.

Nilipoona hivi kengele ya hatari ikaanza kugonga kichwani,wale watu niliona kabisa wanakuja usawa wangu yaani wananikaribia na kwa muenekano wao nilijua kabisa ni wakali wa donta.Mtu kapiga kapelo macho hayaonekani anakutazama kwa kuchungulia kwenye kapelo

Baada ya kukaribiana nao nikaona kama walitaka kunifuata halafu wakasita mimi nikapita zangu baada ya hatua kadhaa nikageuka nikawaona wamesimama wananitizama,mimi nikakaza mwendo,toka siku hiyo sijawahi kupita jangwani kwa miguu giza likiwa limetanda.

Kuhama kwangu kutoka upande mmoja kwenda kwingine kuliniokoa ningekutana nao wangenivamia,japo hata baada ya kuhama walinifuata,wakati nahama kutoka upande mmoja kwenda mwingine sikuwatilia mashaka kama ni watu wabaya, nafsini tu niliamua nibadili upande wa kupita,watu wale wakati nawaona kwa mbali nilijua tu ni wapita njia kumbe ni wapiga roba
 
Mwezi wa 10 mwaka jana nipo home alone, nina stress kali, nimenunua chupa ya konyagi na sigara. Namaliza konyagi nawasha sigara. Navuta nikiwa nimejilaza kitandan. Napitiwa na usingizi. Naamka usiku sana nakuta shuka na neti vimeungua sehem kubwa kidogo. Najiuliza mpaka leo, ni nani alizima ule moto? Hakika nilistaajabu uwepo wa Mungu. Kwa kweli [emoji120][emoji24][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi wa 10 mwaka jana nipo home alone, nina stress kali, nimenunua chupa ya konyagi na sigara. Namaliza konyagi nawasha sigara. Navuta nikiwa nimejilaza kitandan. Napitiwa na usingizi. Naamka usiku sana nakuta shuka na neti vimeungua sehem kubwa kidogo. Najiuliza mpaka leo, ni nani alizima ule moto? Hakika nilistaajabu uwepo wa Mungu. Kwa kweli [emoji120][emoji24][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah umenikumbusha mistari ya darasa "sinzia na fegi uchome kibanda"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Actual kwa Mimi ilikuwa uwoga tuu tulipanda usafiri wa anga Sasa sikuhio hali ya hewa ilikuwa mvua mvua zahapa napale Sasa tulivyoanza safari ule usafiri Ulikuwa unatingishika kama upande usafiri wa ardhini kisha upite kwenye barabara isio nalami yenye mashimo shimo na makokoto ndio Ulikuwa hivyo kwaile safari ya lisaa moja Nilikuwa nimekaa kwa tahadhari kweli maana nilikaa siti usawa wa engine au mabawa ya ndege

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chombo kilipata misukosuko anga la kwamsisi ila s tukafanikiwa kutua salama mapango ya Amboni

Jr[emoji769]
hahaah dah kwamsisi walinitest wife akauona mchezo ila kuna wanawake majasiri sana! wife ananiambia hawa ******* wanakupiga zongo mumewangu basi nikawa napewa maelekezo na mimi nijitutumue,
 
Sitasahau mwanamke alivyonidanganya yupo single kumbe kaolewa katikati ya mgegedo mlango ukagongwa mumewe karudi aisee!!!!! Nauliza nani tena huyo anasema atakuwa mume wangu doh! Gafla nikahisi tumbo la kuhara fastar nikapewa wazo lakuingia uvunguni mwa kitanda
Aise kama unavyoelewa vungu za vitanda vya wabongo wengi vumbi la kutosha yaani dk40za kuwa ndani ya uvungu sitazisahau..yaani chafya imenibana kikohozi kimenibana tumbo la kuhara ndio limechanganya aise,nilimsihi na kumwomba Mungu kwa moyo wa dhati aniepushe na balaa mixer kutubu
Mungu mwema jamaa akakaa kidogo akasema alikuwa mlinzi kumbe na siku ile walipangiwa lindo watu wawili ye akaona arudi tu home kupumzika na mkewe jioni awahi lindoni maana sio mbali na hapo kwake
But mkewe akamwambia vipi ulale huku afu kule mwenzako akavamiwa huoni itaonekana ulipanga njama za wizi jamaa akaelewa somo akasepa'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EvilSpirit,
Hiki tokea dharula Na #uka Lazimika kutembea usiku hasa mitaa yenye vibaka zingatia yafuatayo:

Beba siraha yyte ndogo kama kisu screw driver zile ndefu (bisi bisi) kwa ajili ya kuwa weka sawa vibaka pale maji ya kizidi unga

Hata kama sio mvutaji wa sigara nunua sigara yako moja sports , embassy , au hata nyota SM za wachumba achana nazo

Wakat unatembea na kukaribia eneo lao washa kisha vuta huku #una katiza eneo hilo na tembea kwa kujiamini % zote bila woga

Waarabu wa pemba ujuana kwa viremba na ukifwatwa na kibaka yyte ujue shida yake ni kugongea sigara na sio kukufanyia wizi
 
Nikiwa dalasa la sita siku hiyo niliamua kujisomea usiku, so nilikuwa nasoma kwa kutumia kibatari, nilikuwa nasoma huku nimelala kitandani na kibatari kiko pembeni kidogo juu ya meza, nilipitiwa na usingizi kumbe mto wa sufi niliokuwa nimejiegemeza uliangukia kibatari ukaanza kuwaka na nilikuwa nimelala na babu yangu ambaye alikuwa haoni vzr na kutembea kwa tabu sababu ya uzee pia kilichosaidia huyu babu yangu tulilala vitanda tofauti!

Aise mto wote uliungua babu akaita sana sikusikia sababu ya usingizi mzito makelele ya babu ndio yaliyowaamusha watu wakaja kuvunja mlango godoro la Sufi limeanza kushika moto na chumba kimejaa moshi, aise sielewi ule usingizi ulitoka wapi maana pamoja na makelele ya babu sikusikia, watu waliita sana kwa nje sikusikia hata walivyovunja mlango sikushtuka wakanibeba kunitupa nje ndio nashtuka,
Mpk Leo naamini ni Mungu alitusaidia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]. Hebu amalizie Kwanza afu aeleze anakaa sehemu gan ambazo Hadi nyoka wanazingua vyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
soma komenti zangu namba 3 na 4 nimeshatoa maelezo,hata hivyo nyoka kuingia vyumba sio kitu kigeni inategemea na maeneo,kilichonitisha nyoka alisimama nusu mzima akawa ananitazama pale kitandani na mimi namtazama tukawa tunatazamana,usiombe,akashusha kiwiliwili chake akageuka akaanza kuondoka kuelekeamlangoni kawa kasi,kisha akasepa.
Ni vizuri kuwa na tabia ya kufunga milango ya nje hata kama ni mchana kwani nyoka nyura na hayawani wengine waweza ingia.pia msipende kuweka makorokoro mengi nje ya nyumba,na kupanda maua mengi yaliyosongamana bila kufanya usafi wa mara kwa mara kwani ni hayo ni hifanyi nzuri sana kwa hao.
watu wengi sana waewahi kuomba msaada wa kuua nyoka walioingi ndani mwao.
 
Back
Top Bottom