Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasiokuwa na Seat (wanasimama)

Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasiokuwa na Seat (wanasimama)

Route za kwenda mikoani hasa kuanzia Dar-mbeya, Dar-mwanza Bus nyingi zina haya mambo ya kupakiza abiria inakuwa usumbufu tena
Majuzi nimepanda basi moja zuri linatokea Dar kwenda Manyara kupitia Kondoa.
Seats zao ni 2x2.
Njiani sasa!
Masai na wataturu wananuka samli, wamepakizwa, wengine wamekalia ndoo na wengine wamekaa chini.
Ovyo kabisa.
Baadaye nikaona na kunguni kwenye seat ya mbele.

Usafiri wa kifala sana.
 
Hv bus linakuwaje VIP wakati linasiti 56/54? Huwa nawaambia watu bus likishazidi siti 30 hapo hakuna u VIP. Muda mwingi safarini tunautumia tukiwa tumekaa so nilitegemea ili kuifurahia safari mtu awe comfortable kukaa hata kiasi kujilaza lakini mwisho bus likishakuwa na choo tu ndani lishaitwa VIP
 
Biashara ya Usafirishaji kwa hapa Tanzania walifaulu sana Scandinavia, wengine wanahangaika hangaika bado
Hata KAMATA na RWELE, upande wa luxury na express buses walifanikiwa sana. Na hii ilikuwa ni karne iliyopita.,..

Inashangaza badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma.
 
Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasio na siti

Kuanzia Ally stars BUS wanaoisifia , katarama BUS na Bus zingine nyingi hali hii inafanyia abiria wake.

Unakuta umepanda bus kila abiria amekaa katika seat yake ikifika mahali Bus linaruhusu kupakiza abiria wengine wanaanza kusimama pembeni ya seats za abiria wengine wanakaa katika njia za kupita.

Nini maana ya Bus kuipa Hadhi ya VIP/VVIP?

Wamiliki wa Bus suala hili mnalifahamu?

- Ni bus gani haina tabia hizi?
VIP buses ziko njia ya Dar Arusha na Dar Tanga tu.
Wengine njooni mjifunze.
 
Hao wanaosimamishwa ni maokoto ya wafanyakazi wa bus,malipo yao madogo waoneeni huruma nao wanafamilia zinawategemea.
 
Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasio na siti

Kuanzia Ally stars BUS wanaoisifia , katarama BUS na Bus zingine nyingi hali hii inafanyia abiria wake.

Unakuta umepanda bus kila abiria amekaa katika seat yake ikifika mahali Bus linaruhusu kupakiza abiria wengine wanaanza kusimama pembeni ya seats za abiria wengine wanakaa katika njia za kupita.

Nini maana ya Bus kuipa Hadhi ya VIP/VVIP?

Wamiliki wa Bus suala hili mnalifahamu?

- Ni bus gani haina tabia hizi?
Sema tu mabasi ya kwenda Dar-Handeni ni kero kubwa mtu alipa kabisa na ticket anapewa lakini anasimama toka kituoni mpaka anafika nimeshangaa sana
 
Majuzi nimepanda basi moja zuri linatokea Dar kwenda Manyara kupitia Kondoa.
Seats zao ni 2x2.
Njiani sasa!
Masai na wataturu wananuka samli, wamepakizwa, wengine wamekalia ndoo na wengine wamekaa chini.
Ovyo kabisa.
Baadaye nikaona na kunguni kwenye seat ya mbele.

Usafiri wa kifala sana.
[emoji1787]
 
Pandeni Shabiby gari ya kishua.
Siti nzuri pana,,,
1×2 ila hata upande wa 2,,Kuna space kubwa sana..
Wifi
Kiyoyozi
Mwendo mzuri
Yaani Kuna utulivu wa kutosha.
 
Ninapochoka hizo Bus zinawapitisha abiria wake wakale maandazi moja linauzwa Tsh 2000...
 
Ushamba na ubahili usio na sababu. Mamlaka nazo zimekalia rushwa
 
Njia ya kwenda toilet inafungwa
Wanaosimama wanaegamia siti bus likiyumba unaangukiwa uliyekaa
Wanaegamia siti makalio yakuwa usawa wa kichwa cha abiria aliyekaa unasikia kiharufu kizito kinasambaa puani
Itatuchukua karne kadhaa kuelimika
Hicho "kiharufu kizito kinachosambaa" ni cha nini mkuu.......🤭🤭🤭😄😄😄
 
VIP kibongo bongo bado sana, ndio tunajifunza tuseme ukweli tu... Labda miaka michache ijayo tutafika

Sasa hivi sio ajabu kukuta gari ni VVIP lakini choo kibovu, AC ya magumashi, mwendo wa dereva ni kanyaga twende babaakee, movie zilezile kila siku za mkojani, Ringo, Nagwa... Customer care mbovu, usalama wa mizigo muda mwingine mdogo kwa hiyo ni vuruguvurugu

Kuna bus (Sitalitaja) nilipanda kwenda mkoani nikajutia kutoa hela yangu kwamba nimepanda VIP.
Nyie wenyewe ndio mnatumia mabunzi chooni.
 
Back
Top Bottom