Unakuta tunajenga nyumba bati imeenda juu kupita maelezo ila watoto wanafanyia homework dining room

Unakuta tunajenga nyumba bati imeenda juu kupita maelezo ila watoto wanafanyia homework dining room

Nilidhani Master ni zile zenye en suite bathrooms. Hiyo en suite yenye prayer room ikoje? Ina tofauti gani na Master?

Amandla...
Pengine nimekosea jina lake but nilimaanisha chumba changu cha kulala kina kila kitu humo, hata nilisahau kusema nimeweka mpk kachamber nnayotumia kama ofisi.

Sasa hizi zote haziko kwenye hizo master bedrooms zingine ambazo zina choo na bafu tu.
 
Mimi pia nyumba yangu nilibuni kila kitu mwenyewe.

Kwanza kabisa nilianza kwa ku plan mpangilio wa vitu kwenye kiwanja kabla sijajenga chochote. Nika plan nyumba itakaa wapi, garden zitakua wapi, geti litakua wapi nk. Hii ikaniruhusu nianze kupanda miti, maua nk kabla hata sijaanza ujenzi.

Pili nikaja ku plan nyumba, kuanzia muonekano wa nje, ramani jinsi vyumba vitakavyokua (sebule ikae wapi, master bedroom iwe wapi, jiko liwe wapi, vyumba vya watoto n.k.). Fundi yeye kazi yake ilikua kuweka vipimo vya kitaalam tu.

Aisee kitu kilichokuja kutokea apo sio cha kawaida. Kila mtu akija anasifia mpangilio wa vitu na hii ramani watu kibao wameshakuja kuiomba wakajenge kwao.

Japo pia naelewa sio kila mtu anaweza kufanya ubunifu kama huo.
Exaaaaactly ndo nilichofanya.

Nimehamia hapo just 2023 lakin kuna miti mingi mikubwa. Nilianza kupanda first tree siku ya kwanza nimemaliza kulipia plot. Since then sikuacha kupanda miti ya vivuli, ya maua, ya matunda , na maua yenyewe
Three yrs down the line naishi in a self made jungle. Na ni dar hapa.
Wageni hufika na kupashangaa, na ni kila kitu nimeotesha mwenyewe kuanzia mkiche midogo kabisa usawa wa kiganja, leo ninakula matunda ninafaidi kivuli, mazingira ni daaaaamn! Watu wapande miti aiseeh!
Inaongeza hadhi ya nyumba mno!
 
snowhite naomba nisuggestia miti mizuri ya kivuli na isio na isio chafua mji na matawi mengi.

Karibu sana mkuu
 
snowhite naomba nisuggestia miti mizuri ya kivuli na isio na isio chafua mji na matawi mengi.

Karibu sana mkuu
Midodoma ni best miti kwa kivuli, kutunza ardhi na kubadili hali ya hewa ya eneo. Ukiitunza vizuri ndani ya miaka 3 ni miti mikubwa ya kutoa kivuli, mizizi yake ni salama haifuati nyumba inaenda chini!
 
Ahsante mkuu
 
Nyumba yako inapaswa kudefine aina yako ya maisha!
Nyumba yako inapaswa kuwa ni sehemu unatamani kuwepo zaidi.
Kuwa na goal flan ya makazi!
Kwamba nataka mji wangu uwe hivi, niwe na hiki hapa hapa kuwe na hiki hapa kuwe na hiki.
Itakuchukua muda pengine kufikia lengo, lakini trust me unakuwa na roadmap yako ya kitu unakihitaji!
Mdogo mdogo unafika tu!
 
Pengine nimekosea jina lake but nilimaanisha chumba changu cha kulala kina kila kitu humo, hata nilisahau kusema nimeweka mpk kachamber nnayotumia kama ofisi.

Sasa hizi zote haziko kwenye hizo master bedrooms zingine ambazo zina choo na bafu tu.
Master bedroom ni chumba kikuu ambacho mara nyingi ni kikubwa kuliko vyumba vingine. Siku hizi watu wengine wanakiita chumba hicho Main Bedroom badala ya Master Bedroom. Waswahili mara nyingi wanakiita Masta tu bila kutaja bedroom.

En suite ni chumba kilichomo ndani ya chumba. Maana yake huwezi kuviingia bila kupitia mlango wa kuingia chumba kikubwa. Siku hizi Master Bedroom zina bafu ndani yake. Hilo bafu ndio ensuite bathroom. Mara nyingi vitu kama prayer room, office n.k. zilizo ndani ya chumba cha kulala zinaitwa "attached" k.m. attached study. Lakini unaweza kusema kuviita ensuite study, ensuite prayer room n.k.

Ushauri wangu mwingine ni kuwa kuna hatari sana ya ku personalise nyumba yako kupita kiasi maana inaweza kukuletea changa moto utakapotaka kuipangisha, kuiuza au kuichukulia mkopo. Hata watakao irithi inaweza kuwasumbua. Tusisahau kuwa nyumba ni asset kama mali nyingine.

Amandla...
 
Midodoma ni best miti kwa kivuli, kutunza ardhi na kubadili hali ya hewa ya eneo. Ukiitunza vizuri ndani ya miaka 3 ni miti mikubwa ya kutoa kivuli, mizizi yake ni salama haifuati nyumba inaenda chini!
Kumbe nipande, kuna mtu aliniambia miti yake hufuata nyumba kumbe si kweli.
 
Bati inavyozidi kuinuka ndivyo inavyopunguza rate ya corrosion,kwakuwa muda wa maji kukaa kwenye bati unakuwa mdgo kuliko bati yenye muinuko mdogo,hii hasa inatuhusu sisi tunaonunua mabati ya mchina ya bei rahisi na ubora mdogo...
Hii hai make sense. Ukinunua bati watakuambia minimum slope inayohitajika. Hizi zinazowekwa ni nakshi tu na haziongezi lolote katika kupunguza corrosion. Mbaya zaidi ni matumizi mabaya ya nafasi ya juu ya dari.

Amandla...
 
Nyumba yako inapaswa kudefine aina yako ya maisha!
Nyumba yako inapaswa kuwa ni sehemu unatamani kuwepo zaidi.
Kuwa na goal flan ya makazi!
Kwamba nataka mji wangu uwe hivi, niwe na hiki hapa hapa kuwe na hiki hapa kuwe na hiki.
Itakuchukua muda pengine kufikia lengo, lakini trust me unakuwa na roadmap yako ya kitu unakihitaji!
Mdogo mdogo unafika tu!
Sure.
 
Kumbe nipande, kuna mtu aliniambia miti yake hufuata nyumba kumbe si kweli.
Mimi ningekushauri uandae kwanza ramani ya nyumba ikionyesha pia eneo ambalo ungependa ijengwe. Aidha, barabara, parking, sehemu za maji taka. Baada ya hapo ndio upande miti kuhakikisha kuwa unapata kivuli lakini haizuii upepo na mwanga kuingia ndani ya nyumba.

Amandla...
 
Katika kitu Watanzania wengi hatujui ni ubunifu.

Mimi nyumba yangu ipo tu kinamna haifanani na nyumba yoyote.
Because I made a story when designing it.
Na imetokea kitu kimoja amazing sana.
Haijasha ila one thing najua for sure. Ikiisha ni balaa.
Wengi wamekariri
Nyumba ni jiko, sebule, dining, public toilet, master bedroom , milango 2 ya mbele na jikoni, madirisha na baraza.

Kamaliza.
Yangu iko na kids library, dressing room, milango 3, big windows, balconies 2, ya juu(nimetumia slub ya front porch kuweka balcony juu do kuna ngazi pembeni ya hiyo baraza ya mbele.
Jiko kubwa na ni open kitchen yenye pantry.
2 Master bedrooms na bathrooms kubwa zote kubwa.
1 ensuite yenye prayer room, dressing room kubwa, bathroom kubwa, private balcony yenye view ya migomba na miembe kwa nje, madirisha makubwa sana 3 na security window inayoface main entrance.
See the story?
Nje ni exotic garden ambayo hunisahaulishs kabisa ninaishi Dar es salaam.
Sebule ni kubwa yenye nafasi mno na madirisha makubwa 6.
Ni kweli inanila hela na ninaijenga taratibu sina presha nakaa humo tayari.
Bado skimming, rangi na vioo.
Ila najua ikiisha ah weeeeeh noma sana

Af ndani vitu vichacheee.

Ni uthubutu nilifanya, futa hii vunja hiki , bomoa hii, ila mwishowe its worthy.
Na nilidesign mwenyewe kuanzia mwanzo.
Nimesimamia mwenyewe, ujenzi wa kusimamiwa na sisi wa kinamama mafundi wanatupiga sana ila fresh.
Umesema Sebule ni kubwa na yenye nafasi mno na Madirisha yake Makubwa ndio jumla yapo 6? Hii Sitting ina ukubwa wa vipimo Gani? Yangu Ina 4.5M x 6M Lakini Dirisha ni 3 tu 🥹
 
Back
Top Bottom