Unakuta tunajenga nyumba bati imeenda juu kupita maelezo ila watoto wanafanyia homework dining room

Nilidhani Master ni zile zenye en suite bathrooms. Hiyo en suite yenye prayer room ikoje? Ina tofauti gani na Master?

Amandla...
Pengine nimekosea jina lake but nilimaanisha chumba changu cha kulala kina kila kitu humo, hata nilisahau kusema nimeweka mpk kachamber nnayotumia kama ofisi.

Sasa hizi zote haziko kwenye hizo master bedrooms zingine ambazo zina choo na bafu tu.
 
Exaaaaactly ndo nilichofanya.

Nimehamia hapo just 2023 lakin kuna miti mingi mikubwa. Nilianza kupanda first tree siku ya kwanza nimemaliza kulipia plot. Since then sikuacha kupanda miti ya vivuli, ya maua, ya matunda , na maua yenyewe
Three yrs down the line naishi in a self made jungle. Na ni dar hapa.
Wageni hufika na kupashangaa, na ni kila kitu nimeotesha mwenyewe kuanzia mkiche midogo kabisa usawa wa kiganja, leo ninakula matunda ninafaidi kivuli, mazingira ni daaaaamn! Watu wapande miti aiseeh!
Inaongeza hadhi ya nyumba mno!
 
snowhite naomba nisuggestia miti mizuri ya kivuli na isio na isio chafua mji na matawi mengi.

Karibu sana mkuu
 
snowhite naomba nisuggestia miti mizuri ya kivuli na isio na isio chafua mji na matawi mengi.

Karibu sana mkuu
Midodoma ni best miti kwa kivuli, kutunza ardhi na kubadili hali ya hewa ya eneo. Ukiitunza vizuri ndani ya miaka 3 ni miti mikubwa ya kutoa kivuli, mizizi yake ni salama haifuati nyumba inaenda chini!
 
Ahsante mkuu
 
Nyumba yako inapaswa kudefine aina yako ya maisha!
Nyumba yako inapaswa kuwa ni sehemu unatamani kuwepo zaidi.
Kuwa na goal flan ya makazi!
Kwamba nataka mji wangu uwe hivi, niwe na hiki hapa hapa kuwe na hiki hapa kuwe na hiki.
Itakuchukua muda pengine kufikia lengo, lakini trust me unakuwa na roadmap yako ya kitu unakihitaji!
Mdogo mdogo unafika tu!
 
Bati inavyozidi kuinuka ndivyo inavyopunguza rate ya corrosion,kwakuwa muda wa maji kukaa kwenye bati unakuwa mdgo kuliko bati yenye muinuko mdogo,hii hasa inatuhusu sisi tunaonunua mabati ya mchina ya bei rahisi na ubora mdogo...
Nimeipata hii.
So pengine tutumie ile nafasi kule juu badala ya kuiacha tu?
 
Pengine nimekosea jina lake but nilimaanisha chumba changu cha kulala kina kila kitu humo, hata nilisahau kusema nimeweka mpk kachamber nnayotumia kama ofisi.

Sasa hizi zote haziko kwenye hizo master bedrooms zingine ambazo zina choo na bafu tu.
Master bedroom ni chumba kikuu ambacho mara nyingi ni kikubwa kuliko vyumba vingine. Siku hizi watu wengine wanakiita chumba hicho Main Bedroom badala ya Master Bedroom. Waswahili mara nyingi wanakiita Masta tu bila kutaja bedroom.

En suite ni chumba kilichomo ndani ya chumba. Maana yake huwezi kuviingia bila kupitia mlango wa kuingia chumba kikubwa. Siku hizi Master Bedroom zina bafu ndani yake. Hilo bafu ndio ensuite bathroom. Mara nyingi vitu kama prayer room, office n.k. zilizo ndani ya chumba cha kulala zinaitwa "attached" k.m. attached study. Lakini unaweza kusema kuviita ensuite study, ensuite prayer room n.k.

Ushauri wangu mwingine ni kuwa kuna hatari sana ya ku personalise nyumba yako kupita kiasi maana inaweza kukuletea changa moto utakapotaka kuipangisha, kuiuza au kuichukulia mkopo. Hata watakao irithi inaweza kuwasumbua. Tusisahau kuwa nyumba ni asset kama mali nyingine.

Amandla...
 
Midodoma ni best miti kwa kivuli, kutunza ardhi na kubadili hali ya hewa ya eneo. Ukiitunza vizuri ndani ya miaka 3 ni miti mikubwa ya kutoa kivuli, mizizi yake ni salama haifuati nyumba inaenda chini!
Kumbe nipande, kuna mtu aliniambia miti yake hufuata nyumba kumbe si kweli.
 
Bati inavyozidi kuinuka ndivyo inavyopunguza rate ya corrosion,kwakuwa muda wa maji kukaa kwenye bati unakuwa mdgo kuliko bati yenye muinuko mdogo,hii hasa inatuhusu sisi tunaonunua mabati ya mchina ya bei rahisi na ubora mdogo...
Hii hai make sense. Ukinunua bati watakuambia minimum slope inayohitajika. Hizi zinazowekwa ni nakshi tu na haziongezi lolote katika kupunguza corrosion. Mbaya zaidi ni matumizi mabaya ya nafasi ya juu ya dari.

Amandla...
 
Sure.
 
Kumbe nipande, kuna mtu aliniambia miti yake hufuata nyumba kumbe si kweli.
Mimi ningekushauri uandae kwanza ramani ya nyumba ikionyesha pia eneo ambalo ungependa ijengwe. Aidha, barabara, parking, sehemu za maji taka. Baada ya hapo ndio upande miti kuhakikisha kuwa unapata kivuli lakini haizuii upepo na mwanga kuingia ndani ya nyumba.

Amandla...
 
Umesema Sebule ni kubwa na yenye nafasi mno na Madirisha yake Makubwa ndio jumla yapo 6? Hii Sitting ina ukubwa wa vipimo Gani? Yangu Ina 4.5M x 6M Lakini Dirisha ni 3 tu 🥹
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…