Unamkumbuka Mwalimu wako aliyekufundisha Elimu ya Awali?

Vidudu miaka hiyo ya 80's nilisoma shule ya awali inaitwa Modern Nursery School. Ilikuwa samora kwenye moja magorofa ya msajili mkabala na JM mall ya sasa.
Kulikuwa na mama mmoja muhindi Goa anaitwa Maria Gonzalves. Mungu amrehemu yule bibi alikuwa na upendo wa kipekee.

Primary kuna puuzi moja lilikuwa linaitwa Mkude, alikuwa Olympio ambayo sasa imegawanywa na kuwepo Diamond hapo hapo. Lile kuda lilinipiga fimbo moja ya mgongo mpaka leo nina alama.
 

hahahaa,sema Sir.Mkude.huyu jamaa kataabisha sana watoto watundu.
Siku zote namkumbuka Mama Chiku Mzee na ule mwendo wake wa madaha
 
Mie namkumbuka Mwl Kadebe(madam) , alikuwa mwalimu wangu wa kiswahili Oysterbay primalrly school DSM.(1989) Japo sku faulu darasa ya saba ila yale ambayo alikuwa ANATUASA YA MAISHA tena kwa msisitizo sana mpaka anataka kulia kwamba tuwe na nidhamu, kuzingatia masomo na mambo kama hayo ili kuweza kuyakabili maisha ukubwani.

Kwa kweli nilikuwa simuelewi kabisa kabisa ila sasa ndiyo namuuelewa sana sana nikiwa na zaidi ya 45yrs. Walimu wazamani walikuwa na maono., NAJARIBU KUMPATA KUMPA SHUKRANI ZANGU NIMEKWAMA!!!!
 
Ambao hatukupitia awali tunakomenti wapi?
Anyway ahsante sana mwalimu wangu wa darasa la KWANZA late 1960's.
Ulikuwa mwalimu,mlezi na baba pia. RlP!
 
Std 1 Mwl. Lunyirija, Upanga Primary School.
She is the best😍

Chekechea simkumbuki hata mwalim mmoja ila nakumbuka shule ilikua pale Vijana opp na Mango garden miaka ya 90's.
Hongera mkuu

Miye nataka nikamtafute huyo mwalimu nimpe hata ya soda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…