Mkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:
Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.
Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!
Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.
Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.
Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.