MawazoMatatu
JF-Expert Member
- Sep 6, 2008
- 505
- 63
Labda huyu Dr. Slaa anatakiwa KUAMSHWA. Nimeona tufanye SENSA ya haraka haraka humu ndani ya JF. Kwa wale wote wanaoona DR SLAA agombee mwaka huu basi hebu jiandikishie jina lako tuone mwisho wa wiki tutakuwa wangapi. Tujitokeze kwa wingi ili kumuonyesha Dr. Slaa anavyohitajika.
Dr. Slaa, samahani nimeamua kuanzia jina lako kwa makusudi kabisa maana JEMADARI lazima awe mbele na wengine watafuata.
1. Dr. Slaa 2. MKANDARA 3. King of kings 4. Masanilo kugema 5. Fidel80
6. Bht 7. Tanzania 8. Ndege ya Uchumi 9. Jiwe 10. Jakathesi
11. Technician 12. Kilembwe 13. Ndjabu Da Dude 14. Bollo Yeng 15. Selous
16. Nyamizi 17. Mfwatiliaji 18. Sikonge 19. Ben 20.Lorah
21. Chief 22. Alpha 23. Malunde-Malundi 24. Muhindi 25. Nanu
26. Betina 27. Baija Bolobi 28. Epigenetics 29. Member 911 30. Mlalahoi
31. Mag3 32. Nndondo 33. Tai Ngwilizi 34. Sn2139 35. Shalom
36. Mc 37. Firstlady1 38. Henge 39. Nemesis 40. Mchili
41. Ngambo Ngali 42. Positive Thinker 43. Advocate Jasha 44. Zhule 45. Araway
46. Pasco 47. Mbu 48. The Invincible 49. Vivian 50.
MawazoMatatuMkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:
Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.
Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!
Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.
Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.
Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.
Mkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:
Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.
Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!
Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.
Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.
Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.
haya mkuu,yale yalikuwa maoni yangu tu kutokana na ukweli halisi.naunga mkono yeye kugombea uraisi siku ambayo uchaguzi wa haki utakapo fanyika lakini uchaguzi huu wa sasa hivi bado kabisa na nirahisi kuongeza wabunge wa upinzani sasa hivi kuliko kumpata raisi mpinzani.Arsene Wenger, hata uandike vipi na upinge vipi hilo sisi hatuangalii. Binadamu anayesikiliza maneno ya kuvunja moyo, huwa hafiki mbali. Hakuna aliyejua kuwa Inter Millan itashinda mechi (ifungwe goli moja tu) huku ikiwa na wachezaji 10 na inacheza na Barcelona yenye wachezaji 11. Lakini iliwezekana.
Hata mfanyeje, bado CCM itakuwa na wabunge zaidi ya NUSU. Sasa kwa nini kupoteza muda na UBUNGE wakati ukipeleka mtu Magogoni, atakuwa zaidi ya hao wabunge wote wa upinzani? Kwa nini unaomba kisu kukata mti wakati unaweza kutumia shoka/msumeno ? Kama kucheza faulo, una uhakika gani mwaka huu CCM hawatamchezea Faulo? Tumewazoesha vibaya sana CCM na pia mwaka huu CCM wenyewe wamegawanyika sana na ni kipindi pekee cha kumtandika konde la knock out huyu Tyson muuma watu.