Sielewi watu wanaposema ushabiki wa Simba na Yanga unaharibu mpira wa bongo ,leo Simba au Yanga ikicheza na timu yoyote kwenye ligi kunakuwa na mwamko ,Simba na Yanga wana mataji mengi na udhamini mzuri .
Hata timu zingine zimepata udhamini baada ya makampuni kuona mwamko.
Hivi tukisema Simba na Yanga wanaua wanaharibu mpira wa bongo je ni afadhali tuwe kama derby ya Gormahia na Leopards ambao ni derby lakini derby isiyo na mvuto hata wakicheza hakuna anayeweka attention ,Simba na Yanga wakicheza hadi nchi majirani wanakuja kuangalia mechi.Lakini kuna ligi Kama ya Zambia,DStv inaonyesha haina mwamko kila mechi mashabiki hawafiki hata 1000
Mpira wa bongo unaendelea kwa sababu ya Simba na Yanga ,hata utambulisho wa jezi miaka iliyopita ilikuwa siyo big deal kwa timu za bongo,leo hata Ruvu shooting wanazindua na kufanya press ,tuombe vilabu vingine vipate udhamini mnono wanunue wachezaji wazuri ili ligi ya bongo inoge zaidi.