Unamzungumziaje mchambuzi Geoff Lea

Unamzungumziaje mchambuzi Geoff Lea

Watanzania hawapendi ukweli hapo huyo kijana hajakosea
Kama anaongea kingereza na nyie jifunzeni kingereza
Mpira wa tanzania umejaza mashabiki wasiojitambua ndio kaongea ukweli mmepanic
Ukweli upi hapo, hivi swala kuwa watanzania wanapenda mpira.
Mtu ikilipinga nao ni ukweli?
Kingereza, Unadhani watu wote hawa wanaompinga hawajui kiingereza?

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo comment yupo sahihi kabisa. Ni kweli Yanga au Simba vs Lipuli uwanja ni mapengo tupu. Sema kuliko kuandika negativity hapo bora angepiga kimya tu.
Kaleta ujuaji usiohitajika.
Mtu kapost anaonesha kuwa Tanzania kuna mwamko wa mpira, wadau wachangamkie fursa. Viwanja viboreshwe.
Yeye anakuja na shombo zake, kuwa hizi team zina struggle kujaza viwanja mechi kubwa tu ( akimaanisha hamna mwamko). Asa unajiuliza haya yote ya nini? Ukimhoji anasema ye anaongea Ukweli.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Kuna kikundi cha waandishi kimeibuka, na wanapenda watambulike kama wasema kweli. Lakini kila nikitazama niuone huo ukweli siupati naona ni majungu na chuki tu.
Kwa leo tuanze na huyu GEOF LEA.

Huyu kijana sijui ana shida gani, ni mjuaji hakuna mfano. Bwana Geof lea anaamini kuwa ukosoaji kila kitu ndio kuonesha wewe ni mwerevu na mjuvi wa mambo.

Msimu uliopita alitoa kauli kwamba, haoni simba akifika mahala na beki ile,Mungu si athumani Simba anamaliza makundi amefungwa Goli mbili tu.

Amefikia hatua ya kuanza kusema eti simba na yanga zinatumia Nguvu kubwa kujaza uwanja, na wala sio kwamba mpira unapendwa Tanzania.( hii akizipinga page na wachambuzi wa nje).

Yapo mengi juu ya huyu kijana, naamiini kama na wewe umekutana nayo utasema.

Kama bado hujaona unaweza fuatilia tweet zake.

NB:Hatukatai ukosoaji ila hatutaki Ujuaji.

View attachment 1947012
Ilikuwa vipi akawa mtanzania huyu kijana, tunajua ni mnyarwanda tunaomba vyombo vimfuatilie, imeniuma sana soka letu likichafuliwa, anajiona mjuaji sana kujifanya analijua soka la ulaya mno.Achunguzwe.
 
Kitu gani ambacho ameongea sio cha kweli?
Alivyoreply vile lengo kuu ni kuonesha Tanzania hakuna mwamko wa mpira, je ni kweli?
Huwa siangalii sana mechi za yanga, ila simba mikoa yote aliyopita kajaza uwanja asa unajiuliza huo sio mwamko?
Au unaweza kunisaidia lengo la ukweli wake ni lipi?

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Ilikuwa vipi akawa mtanzania huyu kijana, tunajua ni mnyarwanda tunaomba vyombo vimfuatilie, imeniuma sana soka letu likichafuliwa, anajiona mjuaji sana kujifanya analijua soka la ulaya mno.Achunguzwe.
Ye anakwambia anaongea ukweli, na si mara moja ni mara kadhaa analeta chuki kwenye kivuli cha ukweli.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Mi tangu nilipoona ana swaga za kuweka hereni masikioni sitaki hata kumsikiliza
Kuvaa hereni inategemea na mazingira aliyokulia mtu, kwangu siyo tatizo kabisa.

Hata wanaofuga dread rocks kuna mazingira aliyokulia mtu wala si tatizo na wanaajiliwa kwenye kazi rasmi za maofisini, ila kama hujawahi kutoka nje ya Bongo una haki ya kushangaa hizo swaga ni kitu kigeni.
 
Nimesoma hiyo comment yuko sahihi 100%

Simba na Yanga zinajaza uwanja wa Mkapa kwenye matukio mawili tu

1. Simba/Yanga Day
2. K/Koo Derby

Sisi mashabiki ndio tatizo hapa, kwanini uwanja hatujazi hata kwa 70% tunapocheza na timu kama Ihefu?
Uko Sahihi Kiongozi
 
Tz hamna mwamko wa mpira ila kuna mwamko kwa timu mbili za simba na yanga tu. Simba na Yanga kwenye mechi za ndani hawajawahi kucheza ugenini, maana kokote wanakoenda wanakuta mashabiki wake wamejaa kuliko hata timu mwenyeji. Kaitaba pale kuna uwanja mzuri tu lakini kagera sugar akicheza na mwadui mashabiki hawafiki hata nusu ya wale kwenye mechi dhidi ya yanga au simba.
Prison kahamia mkoani rukwa ambako hakukuwa na timu ambayo inashiriki ligi kuu, lakini prison akicheza na polisi tz mashabiki hawafiki hata nusu ya wale kwenye mechi dhidi ya simba au yanga. Hatupendi mpira ila tunazipenda simba na yanga tu.
 
Tukizipenda simba na Yanga tunakuwa hatupendi mpira?
Au nieleweshe labda unawezaje kuzitenga Simba na yanga na mpira.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Hukumuelewa, yeye alizungumzia idadi ya mashabiki wanaoingia viwanjani wakati Yanga/Simba ikicheza na timu nyingine kwenye ligi, mashabiki ni wachache sana, ukilinganisha na hizo sherehe za wiki ya Mwananchi na simba day ambazo zinakuwa ni special kwa mashabiki wao na pia zinakuwa na promosheni kubwa.
 
Nimemuelewa, unaweza kunisaidia lengo lilikuwa nini?

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Tukizipenda simba na Yanga tunakuwa hatupendi mpira?
Au nieleweshe labda unawezaje kuzitenga Simba na yanga na mpira.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Nchi nzima kuzipenda simba na yanga tu maana yake hao watu wa nchi hiyo wanapenda mpira kwa asilimia chache sana. Shabiki alieko mkoani Rukwa au karibu na mkoani Rukwa ataingia uwanja wa Nelson Mandela kutazama mechi mbili tu kwa msimu mzima. Mechi zenyewe ni Prison dhidi ya simba na dhidi ya yanga.Hapo ni kupenda mpira kweli?
 
Nchi nzima kuzipenda simba na yanga tu ni kupenda mpira kwa asilimia chache sana. Shabiki alieko mkoani Rukwa au karibu na mkoani Rukwa ataingia uwanja wa Nelson Mandela kutazama mechi mbili tu kwa msimu mzima. Mechi zenyewe ni Prison dhidi ya simba na dhidi ya yanga.Hapo ni kupenda mpira kweli?
Kwahiyo hapo hupendi mpira unapenda nini?
Na sio kweli kwamba hizi timu hazina mashabiki.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo hapo hupendi mpira unapenda nini?
Na sio kweli kwamba hizi timu hazina mashabiki.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Point ni kwamba nchi nzima kupenda timu mbili tu sio afya kwa soka.Simba na yanga hawajawahi kucheza ugenini mechi za ndani maana kokote wanakoenda wanakuta mashabiki wamejaa na hivyo kukosa upinzani wa kweli. Hizo timu zingine hazina mashabiki na kama wapo kwa idadi ndogo sana na uthibitisho ni pale zinapocheza dhidi ya yanga au simba.
 
Maoni ya mchambuzi ukiyatilia maanani utateseka bure.
Mwaka 2019 nililiwa fedha ndefu, wachambuzi dunia nzima waliniingiza chaka kwamba liverpool hawezi kupindua matokeo kwa kumfunga barcelona, matokeo yake akashinda liver akashinda 4-0 wakati matokeo yaliyopita barca alishinda 3-0.

Inawezekana alichosema Jeff kwamba kwa beki ile isingefika mbali ila kilichotokea uwanjani ni tabia za mpira tu kuwa na matokeo ya ajabu.
 
Tz hamna mwamko wa mpira ila kuna mwamko kwa timu mbili za simba na yanga tu. Simba na Yanga kwenye mechi za ndani hawajawahi kucheza ugenini, maana kokote wanakoenda wanakuta mashabiki wake wamejaa kuliko hata timu mwenyeji. Kaitaba pale kuna uwanja mzuri tu lakini kagera sugar akicheza na mwadui mashabiki hawafiki hata nusu ya wale kwenye mechi dhidi ya yanga au simba.
Prison kahamia mkoani rukwa ambako hakukuwa na timu ambayo inashiriki ligi kuu, lakini prison akicheza na polisi tz mashabiki hawafiki hata nusu ya wale kwenye mechi dhidi ya simba au yanga. Hatupendi mpira ila tunazipenda simba na yanga tu.
Kwani Simba na Yanga zinacheza unyago siyo mpira ?
 
Point ni kwamba nchi nzima kupenda timu mbili tu sio afya kwa soka.Simba na yanga hawajawahi kucheza ugenini mechi za ndani maana kokote wanakoenda wanakuta mashabiki wamejaa na hivyo kukosa upinzani wa kweli. Hizo timu zingine hazina mashabiki na kama wapo kwa idadi ndogo sana na uthibitisho ni pale zinapocheza dhidi ya yanga au simba.
Sasa unataka mashabiki ulazimishe wapende na vilabu vingine ?

Timu inapendwa kutokana na performance yake uwanjani na namna inavyovutia mashabiki.

Kama Simba na Yanga zimekamata mashabiki wa nchi nzima hiyo inapaswa zipongezwe kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuvutia mashabiki.
 
Back
Top Bottom