Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
Kujitambua ni pamoja na kutunza uliyonayo. Akili yako, hisia zako, roho yako, mwili wako. Na mengineyo.
Ngozi yako ni sehemu ya baraka ulizopewa.
Hivi kweli ngozi yako thamani yake ni kuipaka mafuta ya jero au mafuta ya kula?
Mafuta ambayo sio ya ngozi unapakaje kwenye ngozi yako.
Kama sababu ni umaskini basi uko sahihi. Lakini kama ni mtazamo potofu basi nipo hapa kwaajili ya watu aina yako. Kukuchokoa chokoa hicho kichwa mpaka ubongo wako ukae sawa.
Ni lazima ujipende. Ili wengine wakupende na wakuthamini. Mtu hawezi kukupenda kama hujipendi.
Hata hivyo hujitunzi na kujipenda ili kupata feedback yoyote kwa watu wa nje. Unafanya kwaajili yako.
Vijana, jipendeni.
Mnafanya kazi kwaajili yenu. Msiwe kama mmelaaniwa. Msiwe kama misukule. Msiwe kama watumwa.
Yaani kufanya kazi ufanye wewe.
Alafu kupendeza apendeze mwingine. Zinafanya kazi kweli Kaka?
Ukimpa mwenza wako hela ya mafuta labda ya elfu 50. Wewe paka ya laki moja. Yaani mara mbili yake.
Kama uwezo wako ni elfu 10. Basi mpenzi wako mpe mafuta ya elfu tatu alafu wewe chukua ya elfu saba.
Usiwe na ule mtazamo potofu kwamba mafuta mazuri ni kwaajili ya wanawake. Sio kweli. Mafuta yapo kwaajili ya ngozi. Hakuna ngozi ya kike wala yakiume. Kwenye types za ngozi kwenye urembo kuna ngozi ya mafuta, ngozi mpauko na ngozi ya kawaida.
Mbona meno husemi kwamba dawa ya mswaki ya hivi au vile.
Usiongee kama jitu jinga.
Fuata wataalamu wakuambie.
Ngozi ni yako. Sio ya mtu yeyote.
Jithamini!
Kukomaa kuchoka sio sifa njema. Hyo ni mtazamo wa watu duni. Maskini waliofeli. Wao kufeli ndio sifa. Uchafu ndio sifa. Uharifu ndio sifa.
Mtoto anapozaliwa angalia ngozi yake. Wote wanakuwa na ngozi nyororo.
Hukuzaliwa ukiwa umekakamaa.
Ndio maana unafanya kazi. Kwaajili ya mahitaji yako. Kujitunza na kutunza unaowapenda
Ni laana kubwa kushindwa kutunza ulichopewa na Mungu. Ulichozaliwa nacho.
Unajidharau utegemee nani akuheshimu.
Unanuka utegemee nani avutiwe na wewe. Jipende Bro. Acha mawazo ya kimaskini na kichawi.
Tunza nywele zako.
Tunza meno yako.
Tunza ngozi yako.
Tunza macho yako.
Tunza mwili wako.
Uwe mwanaume unayejipenda. Jitangulize.
Ndio maana mnaambiwa wanawake wanawazidi Akili na upeo.
Mtu mwenye Akili utamuona tuu kwenye yale aliyobarikiwa nayo.
Hivi utajiita unaakili wakati hata kusafisha meno hutaki, kutunza ngozi unaona kama ni ukike wakati ngozi ni yako.
Kama ingekuwa ngozi haipo kwako ingekuwa upo sahihi.
Chochote kilichochako ni wajibu wako kukithamini. Kulingana na hali na kipato chako.
Kipato chako cha milioni moja unapakaje mafuta ya buku mbili aiseeh!
Nimemaliza msijesema jambo ka sentensi moja naandika Biblia.
TaikonMaster
Kwa sasa safarini kwenye Mgodi wa Makunganya, Morogoro