Unapenda kuvaa Kofia? Style gani Unayoipendelea?

Unapenda kuvaa Kofia? Style gani Unayoipendelea?

Screenshot_2026-05-29_223439.jpg
 
Kofia kama accessory, wanaume kwa wanawake wanavaa. Nyingi ni unisex.

Me napenda sana cap, kichwa kama boga lakini still napenda sana. Challenge kubwa ni joto, jasho linajaa sana nikiwa misele Dar.
View attachment 3596002
Kuna hizi za kibabe kama Peaky Blinders ila ukivaa unaonekana dalali, wanavaaga watoto wa mjini. Mi sijawahi zielewa ila kila mtu na fleva yake.
View attachment 3596003
Wadada wakivaaga cap nao wanapendeza, ila kutegemea na mavazi waliyovaa View attachment 3596004
Hizi za wazee wabaka mabaka zinavutia sema ndio ivyo
View attachment 3596005
People who lack confidence often hide behind caps, unless they are cowboys.
 
Makapelo kufunika..

Mie accessories, zimenishinda, sio kofia, sio miwani, saa etc.. kidoogo cheni na bracelet.. navyo nilipewa kama zawadi nikawa na vaa na kuvua, katika kuhama ile bracelet ikapotea nadhani waliiba, silver gram 45, cheni nikaibadili nikamtengenezea mapambo mama watoto.

Ishawahi kutokea nimevaa kofia, cal na kibaghalashia.. ila huwa hazikai kichwani dk 2 nimevaa dk 2 ipo mkonon😂🤣
 
Back
Top Bottom