Unapenda Marekebisho gani yafanyike Polisi na Mahakama

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.
 
Litoke kwenye police force na liwe police service. Askari wengi wa bongo wanaupumbavu vichwani mwao na kupenda kutumia nguvu nyingi kuliko akili hii imepelekea huku mitaani kesi nyingi kumalizwa kienyeji kutokana na kutokuwa na Iman na jeshi lao.
 
Wakoloni walikuwa na jeshi ambao kazi yake ilikuwa kuhakikisha raia asilete fyoko Sasa zile sheria zote za mkoloni hazijabadilishwa hata moja,pendekezo langu badilisha katiba ambayo sheria hizo zimo humo otherwise kupoteza muda
Sheria hizo ziko kwenye Katiba au kwenye sheria zilizounda Jeshi la Polisi??
 
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.
Jeshi la Polisi livunjwe Tuanzishe Jeshi jipya kabisa na hawa wote waliomo waondolewe .
 
Litoke kwenye police force na liwe police service. Askari wengi wa bongo wanaupumbavu vichwani mwao na kupenda kutumia nguvu nyingi kuliko akili hii imepelekea huku mitaani kesi nyingi kumalizwa kienyeji kutokana na kutokuwa na Iman na jeshi lao.
Huko kenya wanaitwa 'Police service',vipi utendaji wao kazi unatofauti na hawa polisi wa Tz?
 
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.
Maboresho ya kwanza ni kuhamisha askari waliokaa mahali pamoja Kwa muda mrefu, haswa kwenye majiji. Wamezoea Sana hayo maeneo hivyo kupelekea wao kupendelea na kutokutenda haki. Mfano hapo Arusha Kuna askari wapo hapo mile, pale central wilayani. Wanasumbua Sana. Muundo mpya wa jeshi hili uendane sanjari na askari wapya. Hamisha gwakisa, Frans, john, OCD, wengi wengi tu. Na hili lifanyike Tanzania nzima
 
Utofauti hapo ni nini??
Police service hii haiitaji matumizi ya nguvu pasipo tumia nguvu mfano watu wanaandamana wewe unaenda kuwapiga risasi wakati ulikuwa na uwezo kuwalinda maandamano Yao yasiharibu aman ya wasio wahusu.
Police force hapa hakuna Cha sheria Wala utaratibu ni mkuu kasema hapana ni hapana piga ua, Yan nguvu inatumika kupita kiasi ata Kwa mambo zinazoitaji usaidiz wao mtu unaogopa tena mda mwingne wanatumia kigezo Cha kutafta ushahidi ama kutuliza aman na matokeo yake ndio Yale ya yule mkuu wao aliesema askari alipiga risasi juu ilampata marehemu
 
Maboresho ya kwanza ni kuhamisha askari waliokaa mahali pamoja Kwa muda mrefu, haswa kwenye majiji. Wamezoea Sana hayo maeneo hivyo kupelekea wao kupendelea na kutokutenda haki. Mfano hapo Arusha Kuna askari wapo hapo mile, pale central wilayani. Wanasumbua Sana. Muundo mpya wa jeshi hili uendane sanjari na askari wapya. Hamisha gwakisa, Frans, john, OCD, wengi wengi tu. Na hili lifanyike Tanzania nzima
😂😂😂😂Kuna watu huwa wanaama na tabia zao usitake kuwapa shida wenzako
 
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.
Kwanza kabisa vigezo vya mtu kuingia upolisi vipitiwe upya. Haiwezekani kwa dunia ya sasa urefu wa mtu ukawa ni kigezo cha kumwajili mtu!

Hivi vigezo vya wakoloni viangaliwe upya na vyote visivofaa viondolewe mapema. Mtu aajiliwe kwa uwezo wa bongo yake/utaifa/uzalendo na vigezo vingine vya kimantiki km ivo. Hapo ndo tunaona mabadiliko chanya vinginevo tusahau mabadiliko ktk geshi letu hili pendwa
 
Waboreshe maslahi ya askari hatutosikia tena mambo ya kubambikia kesi mara sijui rushwa.Siku zote hawa ndugu zetu wanaharibu kazi pale tu linapokuja suala la maslahi.
 
Litoke kwenye police force na liwe police service. Askari wengi wa bongo wanaupumbavu vichwani mwao na kupenda kutumia nguvu nyingi kuliko akili hii imepelekea huku mitaani kesi nyingi kumalizwa kienyeji kutokana na kutokuwa na Iman na jeshi lao.

wewe ni mzigo kuliko hata hao polisi.
kujua tatizo ni 50% ya kulitatua,ila inaonekana hata ubabe wa polisi haijafahamika chanzo ni kipi.

yaani kudhani polisi ni wababe sababu tu wanatumia jina jeshi,ni uzembe wa kufikiri,kaulize kenya hapo,they got romantic name"kenyan police service"ila brutality ni kama imeongezeka.

polisi na matumizi ya nguvu ndio upolisi wenyewe"law enforcement"cha msingi unapokuwa mbele yao jua uko na polisi,ukijizima data utapigwa hata ingeitwa parokia ya kutoa huduma za kipolisi.
 
Mimi nashauri Jeshi la Borish riwaarest chadema wote wanaotusumbua hapa na huko mitaani.

Tunataka kuishi vizuri. Tunenepe.
 
Back
Top Bottom