Unapenda Marekebisho gani yafanyike Polisi na Mahakama

Unapenda Marekebisho gani yafanyike Polisi na Mahakama

Polisi wameachwa huru mno. They have to be regulated and accountable.
 
Police anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha sita + sio hawa wahuni wa kidato cha nne, tuanzie hapo
 
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.

Iwapo CCM itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti, huku hizo taasisi zikiwa sehemu ya kushiriki uovu wa CCM kuendelea kukaa madarakani, usitegemee mabadiliko yoyote ya maana. Ni kweli yanaweza kufanyika mabadiliko kadhaa, lakini sio mabadiliko ya kubadili tatizo la msingi.

Madaraka ya urais yasiyoweza kudhibitiwa na yoyote ndio sababu ya hasa mihimili na taasisi nyingine zote za kimamlaka kuwa dhaifu. Kama rais ataendelea kuwa juu ya sheria, usitegemee mabadiliko yoyote ya maana kwenye vyombo vya dola. Amri kutoka juu ambayo ni toka kwa rais na taasisi yake, ndio yenye nguvu kuliko taasisi yoyote unayoijua hapa nchini.
 
Rais asiteue majaji wala jaji mkuu. Kuwe na tume ya majaji wastaafu. Wao watoe mapendekezo ya mtu anayestahili kuwa Jaji Mkuu, na watu wanaostahili kuwa majaji. Majina ya hao wapendekezwa yathibitishwe na Bunge na kutangazwa na Rais.

Jaji Mkuu au majaji wanapopoteza sifa au kuwa na tuhuma za kuwapotezea sifa, Tume ya majaji wastaafu itaanisha makosa, majina na tuhuma za hao majaji vitapelekwa Bungeni, kisha kwa Rais.

Kuhusu Jeshi la Olisi, kwanza tuanze na uteuzi wa IGP. Majina matatu ya watu wanaostahili kuwa IGPs, yapendekezwe na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wastaafu. Majina hayo yapelekwe Bungeni. Bungeni yapigiwe kura. Majina mawili yaliyopata kura nyingi yapelekwe kwa Rais. Miongoni mwa hayo majina mawili, Rais ateua mojawapo kuwa IGP. IGP atateua makamanda wa mikoa, na hao ndio wawe wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa.
 
Mahakama ijitambue kwamba ni muhimili unaojitegemea

Katiba hii hairuhusu mahakama kuwa Muhimili unaojotegemea, hususan unapokuwa na chama kinachong'ang'ania kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. Ni vigumu sana nchi yenye vimelea vya kijamaa vyombo vyake vya dola, na mihimili kuwa huru. Na mifano ya wazi kuhusu mwenendo huo iko wazi.
 
Maboresho ya kwanza ni kuhamisha askari waliokaa mahali pamoja Kwa muda mrefu, haswa kwenye majiji. Wamezoea Sana hayo maeneo hivyo kupelekea wao kupendelea na kutokutenda haki. Mfano hapo Arusha Kuna askari wapo hapo mile, pale central wilayani. Wanasumbua Sana. Muundo mpya wa jeshi hili uendane sanjari na askari wapya. Hamisha gwakisa, Frans, john, OCD, wengi wengi tu. Na hili lifanyike Tanzania nzima

Je kuna udhibitisho kuwa baada ya kuhamishwa eneo moja kwenda kwingine uadilifu wao ulipanda? Ni kweli kukaa sehemu moja muda mrefu huchangia kufanya kazi kwa mazoea, lakini hii ni kwa watumishi wote wa umma, na sio polisi pekee.

Matatizo ya jeshi la polisi yako zaidi kwenye mwenendo wa upatikanaji wa serikali. Iwapo polisi na hata mahakama zinatumika kama sehemu ya kuingiza serikali madarakani kwa kunajisi uchaguzi, ni wazi kuwa viongozi wanaokuwa madarakani hawataweza kuwabana polisi kutenda kwa weledi, kwani inakuwa ni forumla ya nilinde kwa jua, nikulinde kwa mvua. Kwamba polisi wanasaidia kuwezesha viongozi kuingia madarakani kihuni, kisha serekali ikishakaa madarakani inawaachia polisi nao wavune watakacho.
 
Kuwepo na tume ya kiraia kulisimamia jeshi la Polisi, ku regulate na kudhibiti utendaji wake.
Police oversight commission.
 
Katiba hii hairuhusu mahakama kuwa Muhimili unaojotegemea, hususan unapokuwa na chama kinachong'ang'ania kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. Ni vigumu sana nchi yenye vimelea vya kijamaa vyombo vyake vya dola, na mihimili kuwa huru. Na mifano ya wazi kuhusu mwenendo huo iko wazi.
Nakubaliana na wewe, na madhara tunnayaona mkuu wa nchi anapokuwa m/kiti wa chama anakalia mhimili wa bunge kimabavu. Mbunge analazimika kumpamba raisi bungeni badala ya kumkosoa ili asikate jina lake wakatt wa mchujo. Kaatiba mpya ni muhimu.
 
Maboresho ya kwanza ni kuhamisha askari waliokaa mahali pamoja Kwa muda mrefu, haswa kwenye majiji. Wamezoea Sana hayo maeneo hivyo kupelekea wao kupendelea na kutokutenda haki. Mfano hapo Arusha Kuna askari wapo hapo mile, pale central wilayani. Wanasumbua Sana. Muundo mpya wa jeshi hili uendane sanjari na askari wapya. Hamisha gwakisa, Frans, john, OCD, wengi wengi tu. Na hili lifanyike Tanzania nzima
Polisi wote ni kama vile kabila mmoja, wana utamaduni unaofanana kama vile Wamasai na kula nyama, hawsbadilishiki. Mtoe Arusha mpeleke Mtwara, Bkb, Kgm ...nk, ni walewale, hawabadiliki. Wameshindikana. Inahitajika katiba yenye mfumo mzr wa uteuzi wa viongozi wa mihimili wenye uwezo wa kudhibiti mambo kazini
 
Nataka RPC na OCD wachaguliwe kwa kura kama ma Sherriff wa Marekani


 
Kama unahisi Jeshi la Polisi na Mahakama haviko sawa. Unadhani ni Marekebisho gani yanatakiwa kufanyika ili Jeshi la Polisi liwe bora na Mahakama itende haki inavyotakiwa.
Kuwe na kitengo Cha ufundi ,Kwa ajili ya kutambua ubovu wa gari zilizo barabarani,SII Kwa lengo la kupiga faini,ila kuelekeza na kushauri matengenezo ya lazima,hata ziwepo gereji maalumu,pembeni wa barabara kuu,Kwa afya na usalama wawatumiaji barabara,pia yaweza kuwa chanzo Cha ajira Kwa vijana.
 
Mimi nashauri Jeshi la Borish riwaarest chadema wote wanaotusumbua hapa na huko mitaani.

Tunataka kuishi vizuri. Tunenepe.
Mtu anayeweza kunenepa ni mtu mwenye kuweza kula na kushiba,kama huna meno bilashaka huwezi kula ukashiba,hivyo kumwonea wivu mwenye meno yake SII poa🤔
 
Niache ncheke mie !!
Chawa anapojifanya kuuliza maswali kana kwamba ana ubavu wa kufanya hayo mabadiliko!
We lamba asali tu bwashee ndiyo saizi yako.
 
90% ya mibunge ambayo ndio misimamizi na mitunga sheria yamepata ubunge kwa bao la mkono/wizi wa kura, pale kuna rubber stamp tuu usitegemee chochote zaidi ya maslahi yao, uliwahi kuona wapi speaker wa bunge anajiuzuru kwa sababu kamkosoa Raisi ambayo kiuhalisia ndio kazi yake kusimamia serikali
 
Napenda tu kuwaambia JF mods wasidhani wanatuuza tutaumizwa; wakati wahusika wanataka kujua watu waliotuumiza watulipie kisasi.

That is to say bother hacking everyone kwa sababu ya wivu ukadhani utawaumiza. Kwa wengine ni kupitia ili ili jukwaa we sema unavyotaka ila kuna nafasi jamaa wanatuka kutupa uwezi amini mpaka tunaweka picha zetu.

This is to tell you, you can’t ever hurt me 🤣🤣🤣🤣 natukana thinking you can.

Hujui vigogo wakubwa kweli kweli wanaoulizia development; yaani issue ni mimi.

Uwezi kuniumiza mimi: kuna watu wakijua watakuumiza wewe kwa niaba yangu uamini subiri bye.

I just had to say it na wala sitofuatlia 👋
 
Back
Top Bottom