Unapiga 'gym' na usiku unakojoa kwenye kopo kitaalamu hii tunaitaje?

Unapiga 'gym' na usiku unakojoa kwenye kopo kitaalamu hii tunaitaje?

Salama, upo au ndio ivo tena umeme huu bora kibatari.

Sasa ni hivi kama ilivyo nadra kwa kanali kuogopa kinyonga, una kitambi unaogopa mende, una Nissan Murano, range halafu umepanga kirahisi tu hakuna usawa hapa kama si mizimu basi bombonya fulani by default.

Kijana gym sana, kifua kikubwa, miguu vigimbi as u kno usiku kwa nyumba za kiswahili vyoo n nje mostly, ikiwa utamuona kijana anatoa kopo la mkojo alikojoa usiku yeye kwa akili zake kamili, anaanzaje kuogopa wanaume wenzie kutoka nje kwa mfano? Tafsiri yake ni nini?

Kitaalamu tuiite vipi hii kwa maneno chini ya kumi?
Hii tunaitaga kopoliurinesis
 
Aisee Gym imetafsiriwa vibaya sana
Gym ni sehemu ya kufanya mazoezi ili kuweza kujikinga na magonjwa kama pressure, sukari, magonjwa ya mifupa, magonjwa ya moyo nk
Ubaya ni kwamba watu wengi bado hawajajua umuhimu wakufanya mazoezi na wengi wna tafsiri mbaya sana kuhusu swala la mazoezi.

Wapo watakaosema fanya mazoezi nyumbani, ni kweli inawezekana ila kujisimamia kufanya mazoezi nyumbani ni changamoto nyengine sio rahisi kama ambavyo mtu atasema.

Wapo watakaosema kwanini usikimbie barabarani? hii inawezekana sema kuna swala la usalama, magari ni mengi sio salama kukimbia barabarani pia kuna vibaka , na kumbuka sio kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia kulingana na mwili wako

Uzuri wa Gym
Ni sehemu ya kujipatia connection za kazi, biashara nk
Ni familia ambayo hukuwa nayo
Ni addiction nzuri kuliko kushinda Bar
Gym inakusaidia kuepuka vishawish vingi sana, ukitoka mazoezi mwili unakua umechoka hata akili ya kuwaza upuuzi haipo tena kichwani
Ni sehemu nzuri ya kujifunza vyakula gani ni vizuri kwa kula ili kuiepuka magonjwa nk
Gym husaidia kupunguza stress
Gym husaidia afya ya mifupa na mwili mzima
Gym inasaidia kuongeza ufanisi wako wa kazi na pia uwezo wa kufikiria
Kuna dhana kubwa ambayo watu wengi huamini vijana wa Gym ni malaya sana jambo ambalo sio kweli, mfanya mazoezi hamna kitu anajali kama muonekano wake na afya yake na katika ratiba yake lazima gym iwepo sasa huo mda wakuanza kuhangaika na malaya hawezi kuwa nao.
Gym pia husaidia kurudisha furaha katika ndoa au mahusiano, watu wengi huchukia muonekano wa mume wake au mke wake akinenepeana. Sasa gym inasaidia mtu kurudia muonekano wake wa zamani na hivyo kurudisha mapenzi na ule mvuto uliokuwepo mwanzo katika mahusiano.
 
Akitoka nje kujisadia mtakuja kusingizia alifungua Mlango usiku ili wapangaji wenzie waibiwe


Au atasingiziwa huwa anatoka usiku wa manane kupiga Chabo wenzie…uswahilini kuna mambo mengi sana kwa msiowahi kuishi

Kuna kijana anasema aliwahi kutoka usiku kwenda chooni akakuta Wapangaji wenzie wameinamishana …akajikuta kaingizwa kwny kazi ya kulinda siri maana hakuna anaejua zaid yake…kuanzia hapo akajuta kwanini halali na kopo la kukojolea
Kuna maisha na kuna maisha ya Uswahilini😂😂😂😂
 
Kubeba Chuma na Ujasiri ni viti 2 tofauti. We unadhani Jux anatoka usiku saa 7 akisikia purukushani nje[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom