1. Taarifa za umiliki
Fuatilia kiwanja hicho kinamsoma nani kupitia ofisi za ardhi za eneo husika, pia fuatilia kinamilikiwa kupitia barua ya toleo (letter of offer) au hatimiliki.
2. Historia ya kiwanja
Zungumza na viongozi wa serikali ya mtaa husika, majirani pamoja na wazee wa zamani katika eneo hilo ili kuepukana na migogoro ya kifamilia na mipaka ambayo huenda haijulikani katika ofisi za ardhi.
3. Madeni
Hakikisha una taarifa zote juu ya madeni yaliyopo katika kiwanja hicho kabla hujafanya maamuzi ya kukinunua, fanya official search ofisi ya msajili wa nyaraka wa eneo husika ili ujue kama kiwanja hicho kimewahi kuchukuliwa mkopo pia ujue kama kuna malimbikizo ya kodi ya ardhi ya kila mwaka.
4. Mikataba
Fanya mauziano kisheria mbele ya wakili aliyesajiliwa na TLS, usimpe muuzaji hela cash bali muhamishie muamala kwa ajili ya kumbukumbu zaidi. Pia hakikisha kuna ridhio la mwenza (spouse consent) ikiwa unanunua mali ya wanandoa au kiapo cha muuzaji kukiri kuwa mali hiyo sio ya wanandoa (affidavit) ikiwa mali hiyo sio ya wanandoa.
5. Ziada
Ununuzi wa kiwanja au nyumba una vitu vingi vya kuzingatia kutegemeana na aina ya umiliki wa kiwanja husika, muhimu ni kushirikisha kwanza wataalamu kutoka ofisi za ardhi na mipangomiji pamoja na wanasheria.