Wakuu, si kweli hata kidogo kuwa unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia!!, kimsingi uchawi (hypnotism /mesmerism) ni sayansi, ni field moja kati ya field za sayansi, chukua mfano zama za Issack Newton hadi katika miaka ya 1900 hivi Newtonian mechanics ilikuwa inatawala sana lakini ilifika mahali kulingana na maendeleo ya sayansi duniani Newtonian mechanics ilishindwa kutanzua baadhi ya problems ndipo ikaja modern mechanics ambapo mambo mengi yakatanzuliwa na ugunduzi mkubwa ukafanyika lakini pia tukumbuke kuna mambo mengi leo hii bado ni nadharia tu kwa sababu sayansi ya leo bado haitoshi ku formulate ili kujua ukweli wake na hapa unakuja kuona mapungufu ya sayansi hii leo mfano, nini ni chanzo cha nguvu ya uvutano!!?, jibu lake lipo katika nadharia tu (Einstein general law of relativity ). Halikadhalika uchawi (hypnotism ) ni tawi moja la "elusive science" ambalo kulitanzua na kuliweka wazi watu wameshindwa kwa sababu hawako interested nalo, leo watu wako interested na mambo ya rocket,computer,machineries, nuclear science,nk mambo ambayo ni tangible.
Nadhani itafika muda "uchawi" utakuwa applicable pale ambapo sayansi ya leo itakaposhindwa kutanzua matatizo kama jinsi classical mechanics iliposhindwa na modern mechanics ikachukua nafasi. Hapa tunazungumzia uchawi wa kuleta manufaa (productive) sio ule wa kuua watu nk.