Joseph lebai
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 8,452
- 8,670
Hahaha...Mkuu, hiyo ya tatu ni balaa. zamani tukiwa bado wadogo kuna jirani yetu alikuwa na hiyo sayansi (uchawi) na alikuwa hajifichi kujisema alivyobobea kwenye sayansi hiyo ya Asili. siku moja alikwenda na rafiki yake kuwinda kitoweo poli la BULIGI. kwa bahati mbaya wakavamiwa na simba na yule rafiki yake hakuwa na lakufanya. jamaa akampoteza kwa speed ya radi. jamaa anazinduka anajikuta yuko nyumbani. Asubuhi njema Boss
Tatizo la watu hadi leo hawataki kuamini kama uchawi upo. na watu tulilishwa matango poli sana hasa kwenye dini zetu, mfano sisi wakristo baadhi ya madhehebu wanasema uchawi upo lakini tusiamini.. sasa hapo mm huwa siwaelewagi.. MAZINGAOMBWE NI MOJA WAPO YA UCHAWI, NA KIPINDI CHA NYUMA YALIKUWAGA YANALETWA ADI MASHULENI.. ALAFU LEO MTU ANASEMA HAKUNA UCHAWI.. SHEEEEET.. TUBADILIKE KWA KWEKI, UCHAWI UPO NA JINA LA YESU LINA UWEZO MKUBWA KATIKA HAYA MAMBO.. NAKUMBUKA SIKU MOJA NIKIWA SHULE YA MSINGI.... KUNA MWANAFUNZI MMOJA ALIPAGAWA NA MAPEPO... AKATOKEA JAMAA MMOJA WA IMANI FLAN AKAANZA KUOMBEA, ILA ALIKUWA ANAYAOMBA YALE MAPEPO YAMUACHIE YASIMTESE YULE MWANAFUNZI.. YAAAN ALIKUWA ANAYASUJUDIA YALE MAPEPO, YALE MAPEPO YAKATULIA KWA MDA, NA YAKAMRUDIA YULE MWANAFUNZI TENA TENA KWA NGUVU... ATATOKEA JAMAA MMOJA MLOKOLE AKAYAAMURU YALE MAPEPO KWA AMRI YA JINA LA YESU..... YALE MAPEPO YAKATOKA NDUKI, HAYAKURUDI TENA.. NILISHANGAA SANA WAKATI HUO..
Uchawi haupo katika makaratasi ya serikali lakini kuanzia Ikulu hadi Kitongojini kila binadamu anaamini kuna uchawi. Tatizo dini zimekuja kutupofusha
[emoji120][emoji120][emoji120]zote ni imani tofauti ni moja tu, moja inawakilisha ukuu wa nuru wakati nyingine ni ukuu wa gizaMada imejaa busara na weledi wa hali ya juu . You are a real professor ! Ni kweli wachawi hawajui hesabu lakini wanafanikiwa asilimia mia moja . Faith starts where the reason ends . Imani ya Mungu na uchawi kuna uhusiano gani ?
Mkuu kwani wewe ni mchawi ?Tunasafiri sana mbona!?
Chanzo chako mkuuHapa kwetu usukumani kuna mtu alikuwa akiitwa Ng'wana malundi.na mwingine anaitwa makongolo.hawa watu walikamatwa na mjerumani wakafungwa.lkn kila cku asbh wanawakuta nje.wanafungia tena na kuweka ulinzi mkali.lkn baadae wanawaona wako nje ya gereza.wakiwauliza mmetokaje.wanaaema tumepitia mlangoni.baadae wakawapereka kwenye kisiwa cha mafia wakawaacha huko ili wafe na njaa.wazungu walipoondoka hawa wafungwa wakaulizana.ndugu tutakula nn hapa kisiwani?! Makongoro akasema mm ninaweza kulima ba kuivisha leo hihii,tatzo ni mbegu tutapataje? Mwana malundi akasema mm ninaouwezo wa kupasua hii bahari na tukapita tukitembea.makongolo akasema pasua tufate mbegu za mahindi na malando ili tulime.kweli mwana malundi alitupa kudude kikapasua maji na wakapita mpk ng'ambo.wakachukua mbegu za mahindi na viazi.jioni yake wakapata.kuamka asbh mahindi yameiva na viazi vimechana matuta.ikawa ni kula na kupeleka kuuza mjini kila cku.wajerumani waliposikia kuwa wale wafungwa wanakuja mpk mjini dar es salaam na kuuza mahindi na viazi.ilibidi waje kudhitisha.ba kweli wakawakamatia mjini.na mizigo ya mahindi.wakawaambia tuonyeshini njia mliyopitia.wakaenda ufukweni na kutupa kile kudude maji yakatika na sekende kadhaa wako kisimani.walipofika wakakuta shamba la viaz na mahindi yameiva sana kuliko hata shamba darasa.wakauliza mmepanda lini? Wakajibu tunapanda kila siku jioni na kuvuna kesho asbh.hawa mpk wameacha alama kwenye mawe.km biblia na quruani zingekuwa hazijafungwa.hawa lazima wangekuwemo.
Hapana mimi sio mchawi hata wewe unasafiri sana.... Hapo ulipo vuta picha ya home town kwenu, shule ulizosoma, sehemu ulizotembelea na kufanya kazi.... Unajiona kabisa uko huko lakini kiuhalisia haupoMkuu kwani wewe ni mchawi ?
Wakuu, si kweli hata kidogo kuwa unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia!!, kimsingi uchawi (hypnotism /mesmerism) ni sayansi, ni field moja kati ya field za sayansi, chukua mfano zama za Issack Newton hadi katika miaka ya 1900 hivi Newtonian mechanics ilikuwa inatawala sana lakini ilifika mahali kulingana na maendeleo ya sayansi duniani Newtonian mechanics ilishindwa kutanzua baadhi ya problems ndipo ikaja modern mechanics ambapo mambo mengi yakatanzuliwa na ugunduzi mkubwa ukafanyika lakini pia tukumbuke kuna mambo mengi leo hii bado ni nadharia tu kwa sababu sayansi ya leo bado haitoshi ku formulate ili kujua ukweli wake na hapa unakuja kuona mapungufu ya sayansi hii leo mfano, nini ni chanzo cha nguvu ya uvutano!!?, jibu lake lipo katika nadharia tu (Einstein general law of relativity ). Halikadhalika uchawi (hypnotism ) ni tawi moja la "elusive science" ambalo kulitanzua na kuliweka wazi watu wameshindwa kwa sababu hawako interested nalo, leo watu wako interested na mambo ya rocket,computer,machineries, nuclear science,nk mambo ambayo ni tangible.
Nadhani itafika muda "uchawi" utakuwa applicable pale ambapo sayansi ya leo itakaposhindwa kutanzua matatizo kama jinsi classical mechanics iliposhindwa na modern mechanics ikachukua nafasi. Hapa tunazungumzia uchawi wa kuleta manufaa (productive) sio ule wa kuua watu nk.
Na hakuna hata mchawi aliyejitokeza kubuni au kurndeleza usafiri huo. Pius alitaka wachawi watumie fursa hiyo ya uwezo kuleta maendeleo lakini kwa kuwa wachawi ni waongo walishindwa.Mkuu, kama unakumbuka mwaka 1997 Dr. Matunge aliita wandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali na kuutangazia Umma kuwa anataka kuanzisha huduma ya Usafiri wa Anga kwa kutumia Ungo/sayansi ya asili. Akasema ataanza na ruti ya DAR-MWANZA etc. Kama sijakosea, waziri wa sayansi na technology alikuwa Dr. Pius Ngw'andu. Ilileta hisia tofauti kwa wananchi...
Sijatofautiana sana na huyo jamaa. Zamani wakati nasoma shule ya Msingi mpaka Sekondari nikiingia kwenye mtihani nikiona swali nilikuwa na uwezo wa kukumbuka hiyo topic jinsi Mwalimu alivyokuwa ameandika ubaoni yote. Then nahamisha tu, baadaye hiyo hali ikaja kuisha hii nayo vipi?Kuna ile mada ya telekinesis na mada nyingine ya machale pia mada ya mind reading, nimesahau title zake zinajibu maswali yote
Ila huu ni uwezo na kipawa cha asili cha kujua yajayo
Third eye intuition ulitakiwa kuiendeleza kwa kufanya meditationSijatofautiana sana na huyo jamaa. Zamani wakati nasoma shule ya Msingi mpaka Sekondari nikiingia kwenye mtihani nikiona swali nilikuwa na uwezo wa kukumbuka hiyo topic jinsi Mwalimu alivyokuwa ameandika ubaoni yote. Then nahamisha tu, baadaye hiyo hali ikaja kuisha hii nayo vipi?
Umetisha mkuu! Eti kutunga....na hata kusadikika pia? sasa kama aliyenusurika alikuja to tell the tale, sasa kosa langu kusimulia story liko wapi? Btw, yalishapita ndugu, hayatusaidii tena!Mkuu umejitahidi sana kwa stori nzuri ya kutunga, [emoji2] Unafaa sana kwa uandishi wa stori za kusadikika... Ungekuwa Hollywood basi bila shaka ungekuwa muandishi mzuri wa Filamu za stori na maudhui ya kusadikika [emoji2][emoji2]
Makubwa hii inakuwaje??KuNa hii njia ya kujichinja roho inatoka ndani ya mwili then mwili unaanza kuifukuzia kwa nyuma nmewahi kuijaribu nilitumia sekunde 5 toka Dar hadi visiwa vya comoro kwenye kikao
Kipindi cha nyuma research zote zilizofanyika kuhusu bangi zilikuwa zikija na majib kwamba bangi ni mbaya. Lakini ukweli ni kwamba wanasayansi wengi waliofanya hizo research walikuwa biased toka mwanzo kabisa.
Yaani walikuwa wakienda kufanya research hali ya kuwa wana majibu kuwa bangi in madhara tuu.
Hivi karibuni wamegundua kwamba bangi inaweza kuwa tiba.
(Baadhi ya watafiti waliokuwa wanatoa majib hasi ya matumizi ya bangi wameomba radhi kwa kuwa biased)
Kama wakiamua kuwa neutral na kufanya utafiti (R&D) basi majibu chanya yatapatikana.