Unapokutana na vibaka kuna mambo matatu tu, kimbia sana, uwe tayari kwa pambano au utoe ushirikiano, usianze kuleta ubishi / ujuaji.

Unapokutana na vibaka kuna mambo matatu tu, kimbia sana, uwe tayari kwa pambano au utoe ushirikiano, usianze kuleta ubishi / ujuaji.

Wala usihangaike kuuwa we piga hewani tu
download.jpeg
 
Wakizuzidi nguvu hakikisha mmoja wao anatangulia kwa namna yoyote ile..meno ni siraha kubwa sana ukikamata koo usiachie
 
Kuna siku nina Stress zangu, mchana kweupeee na shati langu la kitenge, nikaona bora niende Beach nikatulie kidogo.

Nimefika nikawa nimekaa nimejiinamia mara nastuliwa na jamaa ananigusa bega, kisha akaniomba 500 ya sigara nikamjibu kuwa sina(hapo mfuko wa kifuani kuna kama buku 2, na simu kitochi)

Nilivyomjibu sina si akaniambia unasemaje Huna wakati hela naziona hapo mfukoni? (Hapo kushoto hakuna mtu na kulia hakuna mtu, beach yote kweupee)

Wakati ananiambia hivyo hapo anatoa bonge la mbisu kiunoni, kwa kuwa nilikua nimekaa na yeye amesimama nikawa mnyonge tu, akakomba vile vichenchi mfukoni, akachukua na simu kisha akachukua na head phones.

Alivyoanza kuondoka nikaanza kumfuata nyuma nyuma kwa tahadhari, akigeuka namwambia, nipe hata line basi, si akajichanganya bhana akawa ananitisha na kisu, nikapiga tikitaka kiwiko chake, kila kisu kikamponyoka kikadondokea baharini kmmmmmmk.

Tulizipiga mtu mbili tu mimi na yule jamaa ile mbaya maana kwa mwonekano alikua kanizidi, ila tulichapana ile kisawa sawa, garagazana sana kwenye michanga, tulivyoachiana nishampokonya vitu vyangu vyote na sendo zake nimekwala nikatoka nduki na yeye akatoka nduki kila mtu anakimbilua upande wake.

Nafika om nikijicheki manundu usoni ila nikajiona mshindi coz vitu vyangu vyote nilichukua kisha nikamsachi na sendo nikabeba
 
Back
Top Bottom