Unapolipa deni kumbuka haya (M-pesa, Tigopesa, Halopesa nk)

Unapolipa deni kumbuka haya (M-pesa, Tigopesa, Halopesa nk)

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
Nazungumzia namna ya kulipa deni ulilorushiwa kwa M-pesa, Tigopesa, halopesa nk. Katika maisha ni kawaida kukwama na kuomba marafiki watunasue na kamkopo.

Mtu anakukopa tuseme laki tano. Unamrushia kwa mpesa (yaweza kuwa mtandao mwingine wowote) laki tano na elfu kumi ili apate na ya kutolea na atimize shida yake ya laki tano.

Kimbembe kinakuja wakati wa kulipa. Jamaa anakurushia laki tano kamili juu ya alama.

Anasahau ile elfu kumi na ada yako ya kumtumia hela. Mbaya Zaidi, bado huwezi kuitoa laki tano yote lazima ukatwe ya kutolea. Kwa wema au tuseme ujinga wako, unaingia hasara ya elfu 15 hadi 20. Hivi akiwa na shida tena utamkopesha mtu wa aina hii?
 
Kiukweli hii hali inakera sana
Mm kuna mmoja hata aje vipi simkopeshi tena mana nilishamwambia kabisa utume na ya kutolea ila wapiii ,, wanakera mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenye akili yake timamu, akikopa laki, siku anarudisha, anatuma angalau laki na elfu kumi. Inakidhi ada ya kumtumia na wewe kutolea hela yako.
 
Yaani inakeraga sana mtu ulikuwa na cash unaweka kwenye simu yako unatuma sh.50 elf na yakutumia siku anarudisha anatuma sh.50 elf tu, hapo unapata sh.ngapi , hata mimi huwa inanikera sana .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu alikuwa ni ndugu yangu.... Hata hakuchukua muda alikuja kukopa tena ....nilimkopeshaa kwa kumpa ukweli ningemnyima siunajua ndugu lawama
Watu wanakosa ustaarabu.Akija tena utamkopesha huyo?
 
Cha muhimu na wewe unatuma bila ya kutolea kama amekuomba elfu 20 basi unatuma hiyo hiyo
 
Mi nilishaachaga hii tabia baada ya kupata hasara, sasa hivi ukiniomba elfu kumi natuma hiyo hyo sahau kabisa kuhusu ya kutolea sijui wala makato.
 
Mwenye akili yake timamu, akikopa laki, siku anarudisha, anatuma angalau laki na elfu kumi. Inakidhi ada ya kumtumia na wewe kutolea hela yako.
Kweli mkuu unaweza hata kubakia na hela ya twist
 
Mi nilishaachaga hii tabia baada ya kupata hasara, sasa hivi ukiniomba elfu kumi natuma hiyo hyo sahau kabisa kuhusu ya kutolea sijui wala makato.
Hasara iko pale pale. Ada wakati unamtumia na ya kutolea upande wako. Ni sawa na unamkopesha elfu kumi unalipwa elfu nane. Ukichaa huu.
 
Hasara iko pale pale. Ada wakati unamtumia na ya kutolea upande wako. Ni sawa na unamkopesha elfu kumi unalipwa elfu nane. Ukichaa huu.
bora , kuliko kumtumia 12,000 halafu ukarudishiwa 10,000.. plus na hayo makato unayosema
 
Back
Top Bottom