Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Nazungumzia namna ya kulipa deni ulilorushiwa kwa M-pesa, Tigopesa, halopesa nk. Katika maisha ni kawaida kukwama na kuomba marafiki watunasue na kamkopo.
Mtu anakukopa tuseme laki tano. Unamrushia kwa mpesa (yaweza kuwa mtandao mwingine wowote) laki tano na elfu kumi ili apate na ya kutolea na atimize shida yake ya laki tano.
Kimbembe kinakuja wakati wa kulipa. Jamaa anakurushia laki tano kamili juu ya alama.
Anasahau ile elfu kumi na ada yako ya kumtumia hela. Mbaya Zaidi, bado huwezi kuitoa laki tano yote lazima ukatwe ya kutolea. Kwa wema au tuseme ujinga wako, unaingia hasara ya elfu 15 hadi 20. Hivi akiwa na shida tena utamkopesha mtu wa aina hii?