Unapomtaarifu mwanamke kuwa mume wake ana mahusiano pembeni unamuharibu kisaikolojia

Unapomtaarifu mwanamke kuwa mume wake ana mahusiano pembeni unamuharibu kisaikolojia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna dada mzuri nikisema mzuri ni mzuri kweli. Aliolewa na mume mwenye kipato cha kawaida na waliishi maisha ya kawaida. Nikimaanisha hakutumia usafiri wa wote mume wake alimnunulia gari, shopping ya nguo za kazini akifanyiwa. Kwakua alikua mzuri alipendeza sana.

Sasa kuna mazee mafisi yenye hela zao yalimtamani sana yule dada. Hawakuwa na access nae kwani hakuwa na mambo mengi. Tatizo alikua mtangazaji wa TV, wengi wakivutiwa kuangalia vipindi vyake hasa wanaume kutokana na uzuri wake na wala si yaliyomo kwenye kipindi.

Mzee mmoja alifanikiwa kumpata mdada aliyesoma na yule mke wa mtu beauty queen. Alimuahidi kumlipa milioni 5 akimuunganisha na beauty queen yule. Kwa shida za mjini dada yule alianza urafiki wa kumtembelea ofisini hadi nyumbani. Beauty Queen alikua decent mno, pakumuanza alishindwa.

Siku alipomwambia mume wako ana cheat, dada aliishiwa nguvu. Alijifanya rafiki bora wa kutoa ushauri na alichomekea na yeye atafute wa kumliwaza kumbe mtu akikuwa stand by.

Masikini mume wa yule dada alikua mhangaikaji katika biashara ili nyumbani mambo yakae sawa. Anasafiri kutafuta nafaka na bidhaa nyingine mikoani. Beauty Queen akianza penzi na Mzee Mwenye ukwasi wake mjini. Siku ya kwanza tu kukutana hotelini mzee alimpa milioni 20 za shopping ili apendeze zaidi.

Hakuna linalojificha chini ya jua, mume wake alikuja kujua na alipoachwa na mume wake Mzee mwenye ukwasi alimwambia scandal ya ndoa yake kuvunjika hataki imhusishe yeye itamharibia image yake na yeye ni mwanasiasa mashuhuri.

Beauty Queen aligundua shost alimdanganya, kwa mume wake yeye ndiye alikua malkia wa moyo wake.
 
Wow kastor katamu embu endelea nn kimetokea! Lete nondo bas hizoo[emoji6]
 
P
Kuna watu wana pesa isiyo na kazi, hapo amemfikiria shopping New York na gharama za hoteli kwa wiki moja.

Bla bla bla bla X 23! Hewa, hizi hadithi Zenu hizi Jaman!

Halafu anampa masharti mtoto wa watu hataki scandal? Who the f""""" is he?

Hizi hekaya zishakuwa nyingi Sana! Have been to NY, you can shop in South Africa, why NY? Why not Las Vegas?

Why not Mliman city? He he he! Some of these stories Bwana! Hamuoni Aibu?
 
P


Bla bla bla bla X 23! Hewa, hizi hadithi Zenu hizi Jaman!

Halafu anampa masharti mtoto wa watu hataki scandal? Who the f""""" is he?

Hizi hekaya zishakuwa nyingi Sana! Have been to NY, you can shop in South Africa, why NY? Why not Las Vegas?

Why not Mliman city? He he he! Some of these stories Bwana! Hamuoni Aibu?

Heee[emoji23]
 
Back
Top Bottom