Habari wakuu,
Kuna jambo limekuwa likinipa mtatizo sana, wakati nakuwa nilikuwa nikipenda sana kusaidia jikoni kwenye mapishi hasa siku ya ubwabwa Maharage, huku nikimuangalia Bi mkubwa akiandaa kachumbari ya kunogeshea ubwaubwa. Inshort hadi sasa napenda sana kachumbari
Niliona Bi Mkubwa akikatakata Vitunguu na kuviosha kwa Maji na Chumvi, nilipouliza akanambia inasaidia kuondoa ukali wa vitunguu, lakini ilipotokea mimi kwenda kuishi kwa Shangazi nilishuhudia uandaaji mwingine tofauti wa Kachumbari, yaani hakuna kusoha vitunguu ni kukatwakatwa kisha kuchanganya kwenye nyanya, nilipouliza nikaambiwa hatuoshi kwa sababu utaondoa virutubisho
Basi leo nimekumbuka kisha nikaanza ku-search kama kuna nakala inayozungumzia hii issue
Nakala hii inasema:
Kila unapomenya na kuosha kitunguu, unaweza kuwa unaharibu virutubisho vyake muhimu kama flavonoids na sulfur ambavyo ni silaha kubwa ya mwili kupambana na magonjwa ya moyo na saratani. Hata hivyo, namna unavyochagua kuiandaa huamua faida utakazopata. Ulaji wa kitunguu kibichi hukupa kiasi kikubwa cha vitamin C na nyuzi lishe ambazo huimarisha kinga ya mwili haraka
Ukichagua kukipika, joto hupunguza baadhi ya vitamin zinazoathiriwa na moto, lakini bado huongeza uwezo wa mwili kufyonza vioksidishi (antioxidants) kwa urahisi zaidi, huku kikifanya kitunguu kuwa laini na rahisi kusagwa. Kwa upande mwingine, uandaaji wa kisasa wa kuchachusha vitunguu (fermentation) huchochea ukuaji wa bakteria walio salama na wazuri wa tumboni (probiotics), jambo linalolinda afya ya utumbo wako na kuongeza nguvu ya kemikali za mimea kuliko kawaida.
Ili kufaidika kikamilifu, jaribu kuepuka kuviosha vitunguu kwa muda mrefu baada ya kuvikata ili visipoteze nguvu yake ya asili. Changanya namna unavyokula—wakati mwingine weka vipande vibichi kwenye kachumbari, wakati mwingine vikaange kidogo kwenye mboga, au jaribu mbinu ya kuvichachusha. Kwa kufanya hivyo, utakuwa unaupa mwili wako mchanganyiko mzuri wa kinga dhidi maradhi.
Chanzo: The Science of Not Washing Peeled Onions for Health Benefits