Unapotuma e-mail kwa Mkurugenzi inamfikia yeye au sekretari wake?

Unapotuma e-mail kwa Mkurugenzi inamfikia yeye au sekretari wake?

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Habari za muda huu ndugu zangu, naomab kujua endapo nitamtumia email mkurugenzi wa taasisi flani ya serikali, je email iyo mfano dg@tcra.go.tz je inamfikia yeye mwenyewe mkurugenzi wa iyo taasisi moja kwa moja na anaisoma au inafikia kwanza kwa msaidizi (secretary wake) the yeye mwenyewe mkurugenzi anapewa taarifa tu na kufanyia kazi. naomba kujua kwenye ili ndugu zangu.

Karibu.
 
wakuu wa taasisi wana ofisi.
hiyo email yako itatua ofisi yake,kama kuna la muhimu yeye pekee kukusaidia atajulishwa,kama ni hitaji la kawaida la taasisini kwake utajibiwa wapi ukawasilishe shida yako.
 
wakuu wa taasisi wana ofisi.
hiyo email yako itatua ofisi yake,kama kuna la muhimu yeye pekee kukusaidia atajulishwa,kama ni hitaji la kawaida la taasisini kwake utajibiwa wapi ukawasilishe shida yako.
kwaiyo kama nikituma email yangu haimfikii yeye mwenyewe kwenye computer yake ya kazi?
 
Yeye Mwenyewe na wasaidizi wake wa karibu wanakuwa na password ya hiyo email, kwenye mataasisi mengine hadi private assistant wake anaweza kuiona secretary wake anaweza kuiona na pia watu wa IT ya taasisi hata watu wa masjala wanaweza kuiona mara nyingi sio yeye peke yake tu anakuwa na access ya hiyo email.
Embu tambua taasisi sio DG tu.
kama unataka yeye mwenyewe tu asome mtumie kwenye email yake binafsi
 
inategemea na utaratibu wa ofisi husika

kuna baadhi ya ofisi kazi ya kupokea mawasiliano kwa njia ya barua pepe huwa inafanywa na wataalam wa kitengo cha IT

wengine hupewa watu wa ofisi ya Public relation ambao huisoma na kuipeleka kwny ofisi inayohusika na jambo hilo wakishalifanyia kazi inapelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji ikiwa na majibu ya hiyo email kwa hatua zake

wengine huwa Personal Assitant wao wafanyie kazi hizo email.
 
Back
Top Bottom