NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Kuna watanzania wengi hasa mikoani bado wanatumia huu mtindo wa kizamani, mali zao zinaishia kuwanufaisha madali.
Mfano mwenye hati ya nyumba anamwambia dalali anahitaji mteja mwenye milioni 10, milioni 1 iwe ada ya udalali lakini dalali anapata mteja wa milioni 30.
Kinachotokea hapo dalali anapiga cha juu milioni 20 pamoja na milioni yake ya ada, mwenye mali atalalamika ila ndio hivyo tena, mlishakubaliana,
ukisema umzunguke ni hatari, Hawa madalali ni watu wajanja wajanja wa mjini, wana mitandao yao unaweza kustukia una kesi ya kumiliki mkia wa twiga (nyara ya serikali)
Unapouza mali yako mpe dalali dau lako kwamba unahitaji mteja mwenye kiasi flani pamoja na ada yake ya udalali, lakini ikija kutokea mteja kapatikana ataelipia zaidi, basi dalali apewe ada yake ya udalali pamoja na asilimia kadhaa katika kilichozidi juu ya bei ya mweye mali ya mwanzo, katika mfano nilioweka dalai apewe ada ya udalali milioni 1 pamoja na asilimia 20 ya milioni 20 iliyozidi ambayo ni milioni 4, jumla dalali apewe milioni 5.