Unapouza mali usimwambie dalali unahitaji kiasi Fulani tu, akipata mteja mwenye dau nono yeye ndie atafaidika kuliko mwenye mali, weka asilimia %

Unapouza mali usimwambie dalali unahitaji kiasi Fulani tu, akipata mteja mwenye dau nono yeye ndie atafaidika kuliko mwenye mali, weka asilimia %

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
1691843212591.png

Kuna watanzania wengi hasa mikoani bado wanatumia huu mtindo wa kizamani, mali zao zinaishia kuwanufaisha madali.

Mfano mwenye hati ya nyumba anamwambia dalali anahitaji mteja mwenye milioni 10, milioni 1 iwe ada ya udalali lakini dalali anapata mteja wa milioni 30.

Kinachotokea hapo dalali anapiga cha juu milioni 20 pamoja na milioni yake ya ada, mwenye mali atalalamika ila ndio hivyo tena, mlishakubaliana,

ukisema umzunguke ni hatari, Hawa madalali ni watu wajanja wajanja wa mjini, wana mitandao yao unaweza kustukia una kesi ya kumiliki mkia wa twiga (nyara ya serikali)

Unapouza mali yako mpe dalali dau lako kwamba unahitaji mteja mwenye kiasi flani pamoja na ada yake ya udalali, lakini ikija kutokea mteja kapatikana ataelipia zaidi, basi dalali apewe ada yake ya udalali pamoja na asilimia kadhaa katika kilichozidi juu ya bei ya mweye mali ya mwanzo, katika mfano nilioweka dalai apewe ada ya udalali milioni 1 pamoja na asilimia 20 ya milioni 20 iliyozidi ambayo ni milioni 4, jumla dalali apewe milioni 5.
 
Pana dalali alisikia nyumba inauzwa milion 100 magomeni akamtafuta mnunuzi akamuulizia milion 200,dalali akainunua kwa milion 100 siku hio hio akaiuza kwa milion 200, mwenye nyumba aliumia sana kuona kapata milion 100 sawa na dalali.
 
Madalali wengi huwa wanaogopa kununua mali hata wakipata mteja mwenye dau nono maana kuna wenye mali huwa ni wao wanatumia watu wengine kumtamanisha dalali ili aingie tamaa anunue yeye, dalali akinunua anakuwa kaingizwa mjini,

Pia nao wateja wengine ni maneno tu, ndio walewale wa 900 itapendeza, jichanganye sasa !
 
Pana dalali alisikia nyumba inauzwa milion 100 magomeni akamtafuta mnunuzi akamuulizia milion 200,dalali akainunua kwa milion 100 siku hio hio akaiuza kwa milion 200, mwenye nyumba aliumia sana kuona kapata milion 100 sawa na dalali.
Udalali bingoo sanaaa...!! Sema ndo uwee mtu wa maneno na connection...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Udalali kama kkoo lazima uwe na rohoo ngumu bila.hivyoo pagumu sanaa
 
Back
Top Bottom