Unapozidishiwa chenji huwa unarudisha au ndio wimbo wa Albert Mangwear "kimya kimya" mwendo wa haraka mbele

Unapozidishiwa chenji huwa unarudisha au ndio wimbo wa Albert Mangwear "kimya kimya" mwendo wa haraka mbele

Nishawahi kurudisha hizi 1000 au 2000.

Nikipata mtihani mkubwa zaidi labda laki 2 na kuendelea nitaleta mrejesho
 
Mwaka 2009 nilitumwa umeme Wa LUKU kipindi hiki umeme ulikuwa unanunuliwa Tanesco tu

Baada ya kupewa elfu tano nikatoa buku kwa ajili ya kununulia Peni na rula sikumuambia MTU .

So ile elfu nne nikaenda nayo kununua umeme

Kufika pale Tanesco yule jamaa aliniwekea umeme wa laki nne

Sasa umeme ulipomaliza muda mrefu bila kukatika watu hawakua wanajua .

Then mwenye nyumba akawa anachukua hela za umeme Kama kawaida huku umeme ukiendelea kuwepo


Kimbembe umeme ulipoisha Tanesco walianza kukata hela yao kila tukinunua .
Nimecheka sana
 
Mpaka konda nimeshawahi kumrudishia.
Kuna kisa kimoja nikishawahi kusema hapa.

Kuna teacher tunajuana aliazima laini yangu ya voda na modem ili atumie.
Kwa kuwa laini haikuwa na salio nikamwambia akaweka MPESA.

Nikaona anarudi ana uso fulani hivi akasema hebu braza tuongee pembeni kwanza, nikasema nini! Akasema dogo kuzidisha pesa kaweka 20,000 badala ya 2,000 kwa hiyo tugawane. Nikasema sio vizuri kwa sababu dogo mwenyewe ni mwajiriwa tu pale itakuwa hasara kwake.

Teacher akamaindi akasema shauri yako, tutakufa masikini.
ticha mpumbavu
hawezi kutajirika kwa 18000
 
Mie niliwai kumuambia wakala niwekee elf 7 ye akaweka elf 70 maeneo ya mwenge yangu nilipogeuka tu nilichukua bodaboda chaaap kuelekea Ubungo, hyo pesa iliyozid nikaibetia na ikaliwa Yote
 
Katika mihangaiko ya hapa na pale unaweza kwenda dukani ama sokoni inapotokea muuzaji kakuzidishia 'chenji" unachukua hatua gani!??

Binafsi huwa narudisha
Wewe je? Wafanyabiashara wanapitia changamoto sana
Kuja tajiri flan tunafanya naye biashara sasa alitakiwa kufanya malipo ya tsh laki8 na 50.

Nipo ofisini kwake na kuna watu kadhaa pembeni wanasubiri huduma kanihesabia pesa harakaharaka kaniwekea mezani.

Nilipohesabu nikakuta ni million moja na elf50 nikahesabu zangu laki8 na nusu then nikampa laki2 zake then nikamwambia boss umezidisha pesa imezd laki2.

Boss alishukuru kinoma na wake jamaa wa pembeni wakaanza kunipa maua yangu.

Mpka leo Boss kanipa acc number yake ya bank nikitaka kudepozit naweka tu napeleka slip na hata hakagui namimi hata simuibii nafanya kazi comfortably na najiamini na yeye anasema ananiamin nisije kumuangusha.

Kifupi now naenjoy matunda ya uaminifu wangu.

Nawashauri muwe na utaratibu wa kurudisha pesa mnapozidishiwa kwani kuna faida nyingi sana kuliko hasara
 
Back
Top Bottom