Salamu kwenu
Huwa siwaelewi watu wanaposema wanafunga wakati kila siku jioni wanakula.
Ninawafahamu watu wengi tu wanaofunga mpaka siku 21 kwa kunywa maji tu na kila siku wanaendelea na shughuli zao.
Mimi mara nyingi tu naenda mpaka siku saba bila kula na kazi nafanya kila siku.
Nadhani wanapaswa kutumia jina jingine lakini sio kufunga.
Funga ina tafsiiri nyingi sana.
Katika kiarabu neno funga lina maana ya KUJIZUIA.
Sasa mtu anaweza akaseema mimi najizuia kula ugali mwezi mzima ila vyakula vingine anakula na akasema amefunga bado yupo sahihi kwa sababu anaingia katika tafsiri ya funga yenye maana ya kujizuia.
Sasa unajjizuia na nini ? Hapo inabaki tafsiri ya mtu husika
Tafsiri yetu sisi waislamu ya kufunga ni kujizuia kula na kunywa na kuingilia kimwili wakati wa mchana,sijui watu munababaika wapi.
Hata wewe mtoa mada unaweza ukaanzisha dini yako ukasema dini yetu kila januari tutajizuia kuingia jamii forum hiyo ndio itakuwa funga yetu kwenye dini hiyo.
Utakuwa upo sahihi kwa mtazamo wako na wala hakuna atakayekupinga kwa sababu neno funga au kujizuia ni pana.
Na kwamba unafunga au kujizuia na nini hapo ndio wataachiwa wahusika wa jambo husika watoe tafsiri yao.
Kwa hivyo mtoa mada ndugu yangu hiyo ndio tafsiri yetu sisi ya maana ya funga.
Usitake kuturekebisha kwamba tutumie jina lingine wakati hakuna pahala tumekubaliana kwwmba kufunga maana yake ni kadhaa wa kadhaa..
Na ndio maana waislamu huwa tunasema uislamu ni dini nyepesi sana kwa mambo kama haya.
Ukifikiria ni kweli yaani kama hii funga mimi nabadilisha ratiba ya kula tu kama alivyosema mtoa mada lakini Mungu ananihesabu nafanya ibada na ananipa thawabu,ama kweli heri ni nyingi katika uislamu.
Ndio maana mtume akasema "umma wangu utaingia peponi isipokuwa mtu atakayekataa mwenyewe.."
Yaani kama hii funga mtu eti hataki kufunga wakati ni kubadilisha ratiba ya kula tu na unajipatia thawabu ila mtu hataki,si kukataa mwenyewe kuingia peponi jamani.