Mkuu
Pantosha , asante sana kwa bandiko hili, ila humu JF ukizungumzia kujiunga CCM... angalia kilichonikuta siku natangaza kujiunga CCM, nilitangaza siku ya tarehe 1 April, bandiko lile likafutiliwa mbali eti ni siku ya wajinga!. Nikatoa ushauri huu
Je, mtu kujiunga CCM ni ujinga? Je, wana CCM ni wajinga? Je, watanzania wanaoichagua CCM, kila uchao ni wajinga? Its not fair
Naunga mkono hoja, na sio hivyo, kwa Tanzania mpaka hapa tulipo, chama cha siasa kwa maana halisi ya chama cha siasa chenye ability, capabilities and the capacity is only one, the one and only CCM!.
Japo nchi yetu ni nchi ya vyama vingi, ukweli halisi wa vyama vingi ni vyama vingi jina tuu, lakini Tanzania ni nchi ya chama kimoja, CCM ambacho sio tuu ni chama pekee cha siasa, bali pia ni chama dola!.
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! kimezungukwa vyama ambayo ni mfano vyama!.
Kufuatia Tanzania kukosa upinzani wa kweli, CCM Itaendelea kutawala milele!.
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Japo kuna watu wana matumaini kuwa one day upinzani utakuja kushika dola, niliwahi kuwaambia
Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla
Na kitakacho ifanye CCM itawale milele ni matumizi ya mbinu zinazoitwa hooks and crooks
CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?
P