Mkuu Paschal Mayalla, nimekutag kwasababu wewe ni mtu unaefahamika. Nataka nikupe neno.
Kila mtu ana haki na Uhuru wa kujiunga na chama chochota cha siasa, hivyo ni haki yako kuwa mwana CCM. Chama uundwa na watu, na si kwamba watu walioanzisha CCM bado ni walewale, hapana CCM unayoizungumzia leo ni tofauti kabisa na CCM ya kina Nyerere. Ni CCM iliyojaa wezi, wala rushwa na viongozi wenye tamaa.
CCM imefikia hatua ya kukiuka misingi ya utawala Bora. Kuna mengi ya kuongea ktk hili lakini ngoja nichomoe moja kwasababu hii thread sikuianzisha Mimi. Bila rushwa, tume ya ovyo ya uchaguzi na matumizi ya nguvu za vyombo vya dola, CCM ya leo haiwezi kushinda uchaguzi. Ni chama kilichochokwa na watu wenye akili.
CCM imefikia hadi kuonga vyeo vya utumishi wa umma kwa wanasiasa. Mwanzoni vyeo vya kiasa vilikuwa uDC na U-RC, lakini kwasasa hadi maDED, Wanajeshi, Mapolice kwa uchache wote wanafanya kazi za siasa za CCM ukiachia mbali aina wasomi Kama Bashiru, Kabudi, Mkumbo nk wanaonunulika kirahisi kwa kupewa madaraka au fedha. Bashiru kwa mf. Ili hali akijua kuwa kosa kubwa, alikubali kutoka ngazi ya juu ya utumishi wa chama kupelekwa ngazi ya juu ya utumishi wa umma. Chama Cha siasa kwenye mfumo wa siasa ya vyama vingi, kinakuwa kimefilisika hivyo utumia giribha na hila. Kinakuwepo madarakani kwasababu ya matumizi ya nguvu na wala si kwasababu ya sera zake wala hicho mnachokiita katiba Bora. Kuwa na sera ni jambo moja lakini utekelezaji wa hizo sera ni jambo kingine. Nakupa mfano mmoja kuonyesha kuwa CCM haina pumuzi ya kuongoza. Nadhani Sasa hivi unaona mambo yanavyoenda ovyo na nchi inaelekea kupigwa mnada (Ndungai). Kwenye ujambazi wa uchaguzi wa 2020 aliofanya JPM na genge lake la kina Bashiru na Polepole, CCM imeshika nafasi zote za uongozi kuanzia vitongoji hadi Raisi. Niambieni, ni jipya lipi imelifanya tofauti na wakati mwingine ambao ingawa kwa kuibiwa kulikuwa na mchanganyiko wa vyama vya siasa kwenye ngazi tofauti za uongozi?
Kwa hiyo ndugu yangu, najua unafagilia CCM kwasababu una jambo lako unalolitafuta, na umelitafuta kwa muda mrefu, siku ukichoka usitulahumu kuwa hatukukuambia. JPM aliteua wengi wasifiaji wake na watukanaji wa viongozi wa vyama vya upinzani, lakini kwa Samia si Sana. Tafuteni njia nyingine.